Saladi Ya Viazi (Potato Salad) Na Mayonnaise (Kachumbari ya Mayai)

Saladi Ya Viazi (Potato Salad) Na Mayonnaise (Kachumbari ya Mayai)

Vipimo

Viazi - 7 vya kiasi

Maharage machanga ya kijani (spring beans) - 1 kikombe

Karoti - 1 kikombe

Mahindi - 1 kikombe

Njegere - I kikombe

Mayonnaise - 3 vijiko vya supu

Kitunguu saumu(thomu/galic) - 3 chembe

Chumvi - kiasi

Pilipilimanga - ½ kijiko cha chai

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Chemsha viazi kiasi (visiive sana hadi kuvurugika).  Kisha menya na kata vipande vidogovidogo, weka kando.
  2. Menya na kata karoti vipande vidogovidogo weka kando.
  3. Chemsha Maharage machanga (spring beans) mahindi na njegere. Karibu na kuwiva tia karoti. Maji ya kuchemshia yawe ya kiasi kidogo tu.
  4. Katika bakuli la kupakulia saladi, weka viazi, na karoti na njegere, maharage na mahindi uliyoyachemsha.
  5. Chuna au saga kitunguu thomu, changanya vizuri na mayonnaise, chumvi na pilipili manga. Kisha mimina katika bakuli pamoja na mchanganyiko wa viazi na mboga/maharage, ikiwa tayari.

Kidokezo:

Karoti na aina za njegere, maharage na mahindi zinapatikana tayari madukani katika freezer, na hazihitaji kuchemshwa sana.

 

 

Share