Saladi Ya Mtindi, Karoti na Tango

Saladi Ya Mtindi, Karoti na Tango

Vipimo

Karoti - 3

Tango - 1 kubwa

*Kitunguu chekundu  au cha majani (spring onion) - 1 kiasi

Mtindi (Yoghurt) - 1 ½ gilasi

Maji - ¼ kikombe

Chumvi - kiasi

Pilipili manga au nyekundu ya unga - ½ kijiko cha chai

Pilipili mbichi - 1

Namna Ya Kutayarisha

Chuna (grate) karoti weka kando

Katakata tango na kitunguu vipande vidogo vidogo

Katakata pilipili mbichi au isage.

Tia mtindi katika bakuli la saladi, ongeza maji kidogo tu kiasi  uchanganye vizuri.

Tia vitu vyote uchanganye vizuri ikiwa tayari.

Kidokezo:

Ikiwa utatumia kitunguu cha majani - tumia kiasi cha misongo (bunch) 3.

 

 

 

 

 

Share