Imaam Ibn Al-Jawziy: Kauli Iliyomliza Kwa Wanafunzi Wake “Ikiwa Mtaingia Jannah Kisha Msinione Humo”

 

Kauli Iliyomliza Kwa Wanafunzi Wake “Ikiwa Mtaingia Jannah Kisha Msinione Humo” 

 

Imaam Ibn Al-Jawziy (Rahimahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Chini ya 'Allaamah Ibn Al-Jawziy (Rahimahu Allaah) walisilimu watu wapatao ishirini elfu miongoni mwao ni Mayahudi na Manaswara na kwa sababu yake walitubia watu wapatao mia moja elfu moja!! Aliandika vitabu vipatavyo elfu mbili!

 

Naye ndie aliyewaambia wanafunzi wake, “Kama mtaingia Jannah (Peponi) na nikawa si miongoni mwenu basi niulizieni na mseme, ‘Ee Rabb wetu kwa hakika mja wako fulani alikuwa akitukumbusha kuhusu wewe’ kisha akawa analia (Rahimah Allaah).

 

 

[Imetajwa na Imaam Ibn Hanbal (Rahimahu Allaah) Katika Dhayl-Twabaqaat Al-Hanaabilah (2/4811)]

 

 

 

Share