Mashairi: Tuwe ni Ahlus Sunnah Si Ahlul Bid'ah

Tuwe ni Ahlus Sunnah Si Ahlul Bid’ah  

 

Kutoka Kwenye Kitabu ‘Makatazo Ya Bid'ah' 

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

Tuwe ni Ahlus Sunnah
Si Ahlul Bid’ah
Tufuate ya Rabbana
Sio yale ya hadaa
Tumtii Nabiyuna
Tukaipate Shufaa
Tuwe ni Ahlus Sunnah
Si Ahlul Bid’ah
 
 
Yale Mola Alosema
Hayo ndio yatufaa
Na alosema Hashima
Si ya kwetu kuzubaa
Lakini Shekhe kasema
Kwa hapo tutaduwaa
Tuwe ni Ahlus Sunnah
Si Ahlul Bid’ah
 
 
Wa kufuatwa Nabiya
Nuru yenye kuzagaa
Ni nani kamzidia
Elimu kwake kukaa
Vipi tutawasikia
Wale waleteao baa?
Tuwe ni Ahlus Sunnah
Si Ahlul Bid’ah
 
 
Hadithi shoti isihi
Hapo hatutashangaa
Bali ndio tufurahi
Kwani ni yetu ridhaa
Na aletaye kebehi
Juu juu twamtwaa
Tuwe ni Ahlus Sunnah
Si Ahlul Bid’ah
 
 
Anayechezea Dini
Kwa ya dunia tamaa
                             Hatumwachi asilani                              
Atamulikwa na taa
Mwisho awe mkononi
Kama ishikwavyo saa
Tuwe ni Ahlus Sunnah
Si Ahlul Bid’ah
 
 
Na achezee lingine
La Dini tunakataa
Kweli shoti tuinene
Bila kuogopa njaa
Na ya Dini yapangane
Ukweli kutapakaa
Tuwe ni Ahlus Sunnah

Si Ahlul Bid’ah

 

 

 
Share