Mkate Wa Sinia/Kumimina Aina Ya 3

Mkate Wa Sinia/Kumimina Aina Ya 3

 

Vipimo

 

Mchele - 2 vikombe vya chai

 

Maziwa - Kiasi

 

Sukari - 1 kikombe cha chai

 

Hamira - 1 kijiko cha chai

 

Ute wa mayai - 2 mayai

 

Tui la nazi - 1 na nusu kikombe cha chai

 

Hiliki - kiasi

 

Mafuta  (ya kupakia treya) - kiasi 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika     

 

  1. Roweka mchele kwenye maji usiku kucha.    
  2. Chuja mchele kisha tia kwenye mashine ya kusagia (blender) usage pamoja na hamira, sukari, hiliki, maziwa na tui la nazi.  
  3. Mimina ndani ya bakuli na ufinike. Weka mahali penye joto ili mchanganyiko uumuke(ufure).   
  4. Kisha tia ute wa yai koroga vizuri .
  5. Paka mafuta kwenye treya au sufuria ya kuchomea kisha mimina mchanganyiko wa mchele .
  6. Choma (Bake) kwenye oveni kwa moto wa 350°C kwa dakika 30-45,  kisha weka moto wa juu (grill) kama dakika 5-10 mpaka ubadike rangi kwa juu.
  7. Utoe kisha ukate vipande pande ukishapoa weka kwenye sahani tayari kwa kuliwa.

 

Share