Swalah Za Sunnah Zote Ni Zipi?

 

SWALI:

Assalamu Aleykum, namshuku ALLAAH alie wapa fahamu ndungu zetu wa alhidaaya kutuelimisha. pia salaamu nyingi zimfikie mtume wetu (s.a.w.) pia nawashukuru sana ndugu zangu kwa iman alhidaaya naomba mutuvumilie namalipo yenu kwa ALLAAH na ALLAAH AWAZIDISHIE ELMU zaidi na zaidi na sasa namshukuru ALLAAH elmu yangu naipata kwa alhidaaya na ninawaamini sana.

bismillah swali yangu.

nimesikia mawaidha kuhusu swala za sunnah sasa nahitaji munielekeze jee imethibiti kutoka kwa mtume S.A.W  nakama ninayo yasema haijathibiti naomba munipe swala sote za sunnah. huyo shekh anasema kuna hadith ya mtume S.A.W. INASEMAATAKAE SWALI SWALA YANJONGEZA KILA SIKU RAKA 12 BASI M.MUNGU ATAHARAMISHA NYAMA YAKE KUTOKANA NA MOTO WA JAHANNAM.

KATIKA SWALA yaalfajir- kuna sunnah muwakala na jua ikitoka una swali swala ya sunnah ya sharuq unaandikiwa unaandikiwa thawabu ya hajj na umra, kabla na baada ya jua kutoka kwa urefu wa mkuki kuna swala ya sunnah baina ya hapo na dhuhri kuna sunna ya dhuha raka 2 mpaka 8 na kuna swala kabla ya dhuhri raka 4 na ukisha swali dhuhri kuna swala sunnah baadiya raka 4, kabla ya kuswali al asir kuna sunnah raka 4 , swala ya maghrib kuna swala  ya sunnah raka 2 na unaweza kuongeza halafu mtume s.a.w alikuwa akiswali raka 4 baada ya isha alafu akilala alafu witri.

 


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola  wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Kwanza tunapenda na sisi kutoa shukurani kwa du'aa zenu nzuri mnazotuombea nyote mnaotuma maswali yenu pamoja na wengineo wanaoingia ALHIDAAYA kutafuta faida mbali mbali. Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aala)   Atutakabalie hizo du'aa na Atuzidishie uwezo wa kuelimishana kwa kadiri Anavyotujaalia. Aamiyn

Tunamshukuru muulizaji kwa Swali lake hili zuri ambalo litampatia mja thawabu za kujichumia kwa ajili ya Akhera yake na kila atakayefuata na kutekelezo hizo Swalah za Sunnah.

Hadiyth uliyotaja haihusiani na kuswali Swalah za Sunnah za idadi ya Rakaa kumi na mbili kwa siku. Kwani hiyo ni kauli iliyokuja katika kuswali Sunnah za kabla na baada ya Swalah ya Adhuhuri pekee kama ifuatavyo:

 عن أم حبيبة رضي الله عنها قالت: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: ((من صلى أربع ركعات قبل الظهر و أربعا بعدها حرم الله على النار)) أبو داود,  الترمذي, النسائي ,ابن ماجه, أحمد والحاكم

Kutoka kwa Ummu Habiybah (Radhiya Allaahu 'anhaa) ambaye amesema: "Nimemsikia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Atakayeswali Rakaa nne kabla ya Swalah ya Adhuhuri na nne baada yake, Allaah Atamupeusha na moto)) [Abu Daawuud, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Ibn Maajah, Ahmad na Al-Haakim]

 

Ama fadhila za kuswali Rakaa kumi na mbili kwa siku imekuja usimulizi ufuatao:

 ((مَا مِنْ عبْدٍ مُسْلِم يُصَلِّي للَّه ِتَعَالى كُلَّ يَوْمٍ ثِنْتَيْ عشْرةَرَكْعَةً تَطوعاً غَيْرَ الفرِيضَةِ ،إِلاَّ بَنَى اللَّه لهُ بَيْتاً فيالجَنَّةِ ، أَوْ : إِلاَّ بُنِي لَهُ  بيتٌ فيالجنَّةِ))   رواه مسلم 

 

((Atakaye Swali Rakaa 12 zisizo za fardhi kwa siku atajengewa nyumba peponi)) [Muslim]

Swalah za Sunnah zote ni kama zifuatavyo:

 

- Sunnah zilizosisitizwa na zisizosisitizwa kama ilivyoelezewa katika ratiba ifuatayo:

NYAKATI ZA

SWALAH

 

*MUAKKADAH  (ZILOSISITIZWA)

GHAYR MUAKKADAH (ZISOSISITIZWA)

KABLA

BAADA

KABLA

BAADA

ALFAJIRI

**2

Soma Suratul-Kafiruun na Ikhlaasw

-

-

-

 

ADHUHURI

 

4

2

-

-

ALASIRI

 

-

-

4

-

MAGHARIBI

 

-

2

Soma Suratul-Kafiruun na Ikhlaasw

2

-

'ISHAA

 

-

2

2

-

 

FADHILA ZAKE:

 ((مَا مِنْ عبْدٍ مُسْلِم يُصَلِّي للَّهِتَعَالى كُلَّ يَوْمٍ ثِنْتَيْ عشْرةَرَكْعَةً تَطوعاً غَيْرَ الفرِيضَةِ ،إِلاَّ بَنَى اللَّه لهُ بَيْتاً فيالجَنَّةِ ، أَوْ : إِلاَّ بُنِي لَهُ  بيتٌ فيالجنَّةِ))      رواه مسلم 

 

((Atakayeswali Rakaa 12 zisizo za fardhi kwa siku atajengewa  nyumba peponi)) [Muslim]

  

(( ركْعتا الفجْرِ خيْرٌ مِنَ الدُّنياومَا فِيها  ))      رواه مسلم.

 

** ((Rakaa mbili (za Sunnah) kabla ya Alfajir ni kheri kuliko duniya na yaliyomo ndani yake) [Muslim]

 

 ((ما من عبد يسجد لله سجدة إلاكتب الله له بها حسنة ومحا عنه بها سيئة ورفع له بها درجة فاستكثروا منالسجود))    رواه ابن ماجه

 

((Mja yeyote atakayesujudu sajda moja ataandikiwa wema mmoja, na atafutiwa baya moja, na atapandishwa daraja yake, kwa hiyo zidisheni kusujudu)) [Ibn Maajah]

Tunakuwekea hapa aina za Swalah za Sunnah zikiwa na maelezo yake mafupi kisha tunakuwekea viungo ambavyo utapata maelezo zaidi kwa kila Swalah:  

 

-         Swalaatul-Witr

Rakaa tatu baada ya Swalah ya 'Ishaa au wakati wowote usiku kabla ya kuingia Alfajiri

Swalah Ya Witr Inaswaliwa Vipi Na Vipi Kutia Nia?

 

-         Qiyaamul-Layl (Tahajjud) hii pamoja na Swalatut-Taraawiyh katika mwezi wa Ramadhaan.

Ni Swalah inayoswalia ima Rakaa mbili au nne au sita au nane na kumalizia na Swalatul Witr.

 Wakati Wa Swalah Ya Tahajjud Na Vipi Kuswali

 

-         Swalaatud-Dhwuhaa

Inaswaliwa baada ya jua kutoka hadi kama nusu saa kabla ya Swalah ya Adhuhuri nayo ni ima Rakaa mbili, au nne, au sita au nane.

Swalah Ya Dhwuhaa - Rakaa Zake, Fadhila Zake na Wakati Wake

Swalah Ya Shuruuq Ni Sawa Na Swalah ya Dhwuhaa?

 

-         Swalaatul-Istikhaarah

Inaswaliwa unapotaka kufanya jambo ukawa hujui kama litakuletea kheri au shari, hivyo unamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Akuongoze katika hili jambo yaani Akuamulie Yeye.

Kwa Nini Tuswali Istikhaarah Na Iswaliwe Kwa Ajili Ya Nini?

 

-       

         

 

Tunatumai kwa maelezo hayo yote utakuwa umepata mafunzo kamili yanayohusu Swalah zote za Sunnah anzoweza kuswali Muislamu katika maisha yake kila siku.

Ama Swalah nyingine za Sunnah ni zile zinazoswaliwa kwa msimu wake, mfano Swalaatul-'Iydayn (Swalah za 'Iyd mbili), Swalaatul-Kusuuf (Swalah ya kupatwa jua au mwezi) Swalaatul-Istisqaa (Swalah ya kuomba mvua) na Swalatul-Janaazah ambazo ni fardhwu kifaaya (fardhi inayotosheleza ikiwa itaswaliwa na Waislamu wengine). 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share