Hummus (Shaam)

Hummus  (Shaam)

 

Vipimo:

Dengu (chick peas) - *1 Kopo kubwa au vikombe 2

*Twahiynah - 3 Vijiko vya supu

Mtindi - 1 kijiko cha supu

Kitunguu saumu(thomu/galic) - 3 Chembe

Ndimu -1 kijiko cha supu

Chumvi - 1/2 kijiko cha chai

Mafuta ya zaytuun (olive oil) -3 vijiko vya supu

Namna ya Kutayarisha:

  1. * Dengu ikiwa sio za tayari, roweka, uchemshe ziwive.
  2. Tia katika mashine ya kusagia (blender) dengu, twahiynah, mtindi, thomu, ndimu na chumvi usage hadi isagike.
  3. Mimina katika sahani yenye shimo.
  4. Nyunyizia mafuta ya zaytuun.
  5. Pamba upendavyo kwa zaytuun au dengu zenyewe au kotmiri.

Kidokezo:

* Twahiynah = ufuta uliosagwa unauzwa tayari katika kopo.

Sosi inaliwa na mkate wa kiarabu (Pita pan bread).

Unaweza kutumia kwa kutengenezea shawarma au kutolea na kitoweo chochote kikavu kama kuku, nyama ya kuchoma, kababu n.k.

 

 

Share