Mtabbal Wa Bilingani

 

Mtabbal Wa Bilingani

 

Vipimo

 

Bilingani 2 saizi kubwa

Twahiynah (paste ya ufuta) – ¼ kikombe

Mtindi -  vijiko 3 vya kulia

Thomu (saumu) – chembe 3 - 5

Chumvi kiasi

Ndimu – 1 kijiko cha kulia

Mafuta ya zaytuni (olive oil) – vijiko 3 vya kulia

 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika   

 

  1. Kata kwa urefu mabilingani mapande mawili.
  2. Weka katika treya isyoganda uchome (Bake) katika oven.
  3. Yakiwiva epua kisha kwangua nyama ya bilingani na utupe  maganda.
  4. Weka bilingani ilokwangua katika mashine ya kusagia (blender)
  5. Tia twahiynah, mtindi, thomu, ndimu, chumvi, usage.
  6. Mimina katika bakuli uchanganye na mafuta ya zaytuni ikiwa tayari kuliwa kama sosi pamoja na mikate na vitoweo kama mishkaki, kuku choma na kadhaalika.

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

 

 

 

 

Share