Saladi Ya Maharage Na Mtindi

Saladi Ya Maharage Na Mtindi

Vipimo

Mchangnyiko wa maharage yaliyochemshwa - 2 Vikombe

Nyanya - 1 kubwa

Pilipili boga - ½

Kitunguu maji chekundu - 1

Celery - 1 mche (stick)

Parsley (aina ya kotmiri) - 1 msongo (bunch)

Mtindi (yoghurt) - 1 ½ kikombe cha chai

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 1 kijiko cha chai

Maji - ½  kikombe

Chumvi - kiasi

Namna Ya Kutayarisha

  1. Katika bakuli, tia mtindi, changanya vizuri na maji na chumvi.
  2. Tia thomu uliyosaga.
  3. Katakata nyanya, pilipili boga, kitunguu maji, celery na parsely, vipande vidogodogo.
  4. Tia mchanganyiko wa maharage.
  5. Nyunyizia jiyrah (cummin powder)
  6. Tayari kuliwa na mikate ya pita au wali wa mboga.

Kidokezo:

Ukipenda unaweza kukatia pilipili mbichi vipande vidogo au sagia pamoja na thomu.

 

Share