Makaroni Ya Tuna

Makaroni Ya Tuna

Vipimo

Makaroni - 250 gms

Samaki wa Tuna - 3 vibati

Kitunguu - 1

Nyanya - 2

Nyanya kopo (paste) - 2 vjiko vya supu

Pilipili mboga - ½

Pilipili manga - 1 kijiko cha chai

Kotmiri (coriander) - ½ kikombe

Mafuta - ¼ kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Chemsha makaroni kama inavyoashiria paketi au hadi yaive lakini yasivurugike Chuja maji weka kando.
  2. Katakata kitunguu, nyanya, pilipili mboga, kotmiri weka kando.
  3. Tia mafuta katika sufuria, weka motoni. Kaanga kitunguu hadi kigeuke rangi ya hudhurungi.
  4. Tia nyanya, nyanya kopo, pilipili manga, chumvi, kaanga kidogo
  5. Tia tuna, pilipili mboga na kotmiri, kaanga kidogo tu kama dakika moja tu, zima moto.
  6. Changanya na makaroni vizuri ikiwa tayari.

  

 

 

 

 

 

 

Share