Chatine Ya Embe Mbichi

Chatine Ya Embe Mbichi 

Vipimo

Embe Mbichi - 4  

Pilipili mbichi - 2

Pilipili mbuzi - 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) - 3 chembe

Chumvi - kiasi

Sukari - 2 vjiko vya chai

Namna Ya Kutayarisha

  1. Menya embe mbichi, katakata vipande vipande.
  2. Tia vitu vyote katika mashine ya kusagia (blender) tia saga kwa maji kidogo tu kiasi cha kusagia.
  3. Mimina katika bakuli ikiwa tayari kuliwa na chakula chochote upendacho.
Share