Saladi Ya Fattuwsh -2 (Lebanon)

Saladi Ya Fattuwsh -2  (Lebanon)

Vipimo

Majani ya saladi aina yoyote - 1 Msongo

Kitunguu maji - 1

Nyanya - 1

Tango - 1

Pilipili tamu jekundu - 1

Nanaa (mint leaves) - 7 – 10 miche

Parsely (aina ya kotmiri) - 1 msongo (bunch)

Mkate wa pita mkubwa - ½ (kata nusu yake)

Sosi (dressing) yake - ¼ kikombe cha chai

Namna Ya Kutayarsiha Na Kupika

 1. Osha vizuri majani yote, weka kwenye chujio yachuje maji yote.
 2. Katakata majani ya saladi, parsely, nanaa  weka katika bakuli.
 3. Katakata kitunguu, nyanya (chopped) tia katika bakuli.
 4. Katakata tango, na pilipili tamu (cubes) tia katika bakuli.
 5. Changanya vizuri vitu vyote.
 6. Katakata mkate wa pita vipande virefu refu kisha weka katika treya.
 7. Choma (grill) katika oveni hadi vigeuke rangi.
 8. Epua ukatekate vipande vidogodogo kama kwenye picha.
 9. Karibu na kula tia sosi  (dressing) katika bakuli la saladi uchanganye vizuri.
 10. Chaganya na vipande vya mkate kidogo na vinginevyo weka juu ya bakuli ikiwa tayari.

Sosi (dressing) Ya Fattuwsh

Kitunguu saumu(thomu/galic) - 3 chembe

Sumac (ndimu nyekundu ya chenga) - 1 kijiko cha supu

Pilipili nyekundu ya unga - 1 kijiko cha chai

Mafuta ya zaytuni (olive oil) - 2 vijiko vya supu

Siki - 1 kijiko cha supu

Namna ya kutayarisha Sosi ya Fattuwsh

 1. Chuna au katakata kitunguu thomu vipande vidogogo mno (chopped) weka katika kibakuli cha kiasi.
 2. Tia vitu vyote vingine uchaganye vizuri.
 3. Tumia katika saladi kama ni dressing yake.

 

 

 

Share