Saladi Ya Vitunguu Na Pilipili Mboga Tofauti

Saladi Ya Vitunguu Na Pilipili Mboga Tofauti 

Vipimo

Saladi la duara - 1

Tango - 1

Pilipili mboga jekundu - ½

Pilipili mboga kijani - ½

Pilipili mboga manjano - ½

Karoti - 1

Kitunguu cha zambarau (red onion) - ½

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Katakata saladi la duara lioshe, lichuje na lipange katikati kwenye sahani.
  2. Katakata matango slesi yapange kuzunguka sahani.
  3. Kuna (grate) karoti kisha mwagia juu ya saladi kisha katakata mapilipili mboga tupia tupia  juu ya karoti.
  4. Kata kitunguu slesi kisha tupia tupia juu.

Kidokezo:

Ukipenda changanya ndimu , mafuta ya alizeti (olive oil) na chumvi mwagia juu.

 

Share