Taraawiyh: Akiondoka Kabla Ya Imaam Kumaliza Rakaa 20 Akaswali Witr Nyumbani Atapata Fadhila Za Qiyaamul Layl?

 

 

Akiondoka Kabla Ya Imaam Kumaliza Rakaa 20

Na Akiswali Witr Nyumbani Atapata Fadhila Za Qiyaamul Layl?

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

As-salamu Aleikum,

 

Naomba munisimuliye kuhusu swalah ya taraweeh misikiti mengine wanaswali rakaa 23 na na mimi ni mtu wa kuswali 11 pamoja na witry kama ilivyo katika sunnah.Je nikiswali 8 pamoja na imam nikamaliziya witry nyumbani nitapata ujra huu alosema mtume sallahu alayhi wassallam.

kutokukamalisha Swalah ya taraawiyh na Imaam ili kupata fadhila za Qiyaamul-Layl kwani Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

amesema:

 

((Atakayesimama (kuswali) na Imaam hadi amalize ataandikiwa (fadhila za) Qiyaamul-Layl)) [Imesimuliwa na at-Tirmidhiy na kaipa daraja ya Swahiyh al-Albaaniy katika Swahiyh at-Tirmidhiy]

 

 Sallahu Aleyhi Wasallam.

 

 

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Tunashukuru kujua kwamba unafuatilizia vizuri na kwa karibu mafundisho

kwenye tovuti yako. Tunamuomba Allaah Akuzidishie elimu.

 

Kwa mujibu wa Hadiyth hiyo, tunaona kuwa hutokuwa umeswali na Imaam hadi mwisho na hivyo kuweza kupata fadhila zilizotajwa humo kwani bado Imaam atakuwa anaendelea kuswali sehemu ya Swalaah hiyo na wewe ushaondoka.

 

Unachoweza kufanya ili usikose fadhila hizo, ni kama walivyosema ‘Ulamaa kuwa unaweza baada ya Imaam kutoa Salaam katika Swalaah ya Witr, wewe kunyanyuka na kuswali Rakaa moja ya kuitengua ile Witr na hapo utakuwa umefanya mawili kwa wakati mmoja. Utakuwa umekamilisha Swalaah na Imaam hadi mwisho, na pia utaweza kwenda nyumbani kuswali Swalaah yako ya Witr. Na hiyo ni kwa sababu hakuna Witr mbili katika usiku mmoja kama alivyosema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

((لا وتران في ليلة)) رواه الترمذي

((Hakuna Witri mbili katika usiku)) [At-Tirmidhiy]

 

Pia imethibiti kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa baadhi ya nyakati si kila mara, akiswali Rakaa mbili baada ya kuswali Witr japokuwa alishasema kuwa Witr iwe ndio Swalaah ya mwisho ya usiku.

 

Tafadhali bonyeza kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi.

 

Kuongeza Raka'ah Moja Baada Ya Witr Na Imaam

 

 

Na Allaah Anajua zaidi  

 

Share