Saladi Ya Bilingani Na Parsley

Saladi Ya Bilingani Na Parsley

Vipimo

Bilingani - 3

Matango - 3

Nyanya/tungule - 3

Kitunguu - 2

Parsley (aina ya kotmiri) - 5 misongo (bunches)

Mafuta ya kukaangia

Namna Ya Kutayarisha

  1. Katakata bilingani vipande vya  mraba (cubes) kisha kaanga katika mafuta.
  2. Epua na chuja mafuta kisha weka katika bakuli la saladi.
  3. Katakata matango, nyanya/tungule, kitunguu.
  4. Katakata parsely kisha changanya vizuri.
  5. Wakati wa tayari kula tia dressing (sosi ya saladi)

Vipimo Vya  Sosi Ya Saladi (Salad Dressing)

Kitunguu saumu(thomu/galic) - 3 chembe

Pilipili mbichi - 1

Siki au and ndimu - 3 vijiko vya supu

Chumvi - kiasi

Namna Ya Kutayarisha

  1. Chuna (grate) au saga kitunguu thomu, kisha weka katika kibakuli.
  2. Katakata pilipili mbichi (chopp) tia kwenye bakulia
  3. Changanya na viungo vilobakia.
  4. Wakati wa kula, mwagia juu ya saladi uchanganye vizuri ikiwa tayari.
Share