Kufukiza Ubani Na Mwanamke Kukaa Arubaini Anapojifungua Inafaa?

 

Kufukiza Ubani Na Mwanamke Kukaa Arubaini Anapojifungua Inafaa?

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Nimesoma kuwa kuchoma ubani ni mila ya makafiri walioingia ktk uislam lakini ktk usilamu hakuna arobaini ila kwa mama aliyejifungua tu hebu nipe ufafanuzi.

 

 

JIBU

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Sisi Waislamu tumepata neema ya kuwa Dini hii yetu imekamilishwa na Yeye Mwenyewe Muumba wetu, Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  kama Alivyosema:

 

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمْ الْإِسْلَامَ دِينًا

Leo Nimekukamilishieni Dini yenu na Nimekutimzieni Neema Zangu kwenu na Nimekuridhieni Uislamu kuwa ni Diyn yenu [Al-Maaidah: 3]

 

 

Kwa ajili hakuna nyongeza juu ya yale aliyokuja nayo Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wala kupunguzwa. Kinachoongezwa au kupunguzwa ni kile kilichokuwa na kasoro ndani yake sio kilichokamilika.

 

 

Hakuna mafunzo ya Dini kuhusu kufukiza ubani, na kwa maelezo zaidi ingia katika kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:

 

 

Kufukiza Ubani Wakati Wa Kuomba Duaa Inafaa?

 

 

Ama tukija katika arobaini, ni kuwa arobaini kwa mwanamke aliyezaa ni ada na sio Dini. Hiyo ni kwa sababu wamechukulia kauli ya kuwa damu ya nifasi baada ya mwanamke kuzaa mwisho ni lazima iwe siku arobaini. Lakini hakika ni kuwa damu hiyo inaweza kukatika na kwisha hata kwa masaa machache na baada ya hapo asione tena damu na mara nyingine inaweza ikamchukua yeye akiwa katika damu hiyo ya uzazi siku arobaini au zaidi ya hapo au chini ya hapo.

 

 

Akiona hivyo, kuwa damu yake imesimama, ikiwa ima ni baada ya masaa au siku chache mwanamke mzazi ni lazima ajitwahirishe na baada ya hapo afanye ‘Ibaadah zake zote kama Swawm na Swalaah.    

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share