Ni Jemedari Yupi Wa Kiingereza Aliweka Himaya Ya Kiingereza Jerusalem Na Kusema Leo Vita Vya Kikrusedi Vitaisha?

SWALI:

 

ASALAM ALEIKUM

JEMEDARI GANI WA KIENGEREZA ALIINGIA JERUSSALAAM KUWEKA CHINI HIMAYA YA KINGEREZA NA KUSEMA LEO NDIO VITA VYA KIKURUSEIDA VITAISHA?

 

NAOMBA MAJIBU KWENU NDUGU ZANGU WAISLAMU MUNGU ATAWAZIDISHIA WEBSITE HIII YA KIISLAMU IENDELE...AMIN MUNGU ATUPE IMANI WAISLAMU WOTE NA ATUJAALIE TUWE KATIKA JANNATUL FIRDAUS

 

SHUKRAN

 


 

 

JIBU:

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu jemadari wa Kiingereza aliyeitia al-Quds (Jerusalem) katika himaya ya Uingereza. Kabla hatujataja jina lakeni vyema turekebishe kuwa jemadari huo alisema vita vya Msalaba (Crusader) vimeisha na sio vitaisha.

 

Jemadari huyo alikuwa anaitwa Allenby na alisema maneno hayo katika eneo la ndani la Msikiti wa Aqswa tarehe 9 Desemba 1917.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share