Maulidi: Mume Anakesha Maulidini Hataki Kupokea Nasaha Za Mke Afanyeje?

 

Maulidi: Mume Anakesha Maulidini Hataki Kupokea Nasaha Za Mke Afanyeje?

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Je Nifanye Nini Au Nitumie Mbinu Gani Ktk Kuondoa Kero Ktk Ndoa Yangu? Maana Mume Wangu Hupenda Kwenda Maulidini/ktk Madufu Kila Wikiend Na Hii Imekuwa Kero Kubwa Kwangu Isipokuwa Kila Nikimkataza Hawachi Tabia Yake Hii, Na Hii Afadhali Ingekuwa Ndio Kazi Yake Tunayoitarajia Kwa Ajili Ya Kutafuta Rizki La Hasha Ni Mfanyakazi Wa Serikalini Ila Anapenda Tu Madufu Kila Wikiend Hulala Nje Hukesha Madufuni Naomba Msaada Wenu Nitumie Mbinu Gani Kumdhibit Ktk Hili? Wahadha S Salaam Alykum Warahmatullah Wabaarakatuh

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

Uhakika wa tatizo hilo na mengineyo ya wanandoa ni kuwa hatukuchua tahadhari za kutosha kabla ya kuingia katika ndoa hiyo ya sheria. Tatizo hili limekuwa sugu katika jamii kwa kiasi ambacho maswali haya yamekithiri sana. Na kila wakati tumekuwa tukikariri njia ya sawa ya kuchagua mke au mume, njia ambazo zimekuwa hazitumiki na mara nyingi wenye kudhulumiwa katika ndoa hiyo ni wanawake.

 

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametunasihi sana tuwe ni wenye kuchaguana kwa misingi ambayo hatutakuwa na shida kama hizo baadaye katika maisha lakini sisi tumekazana kufuata sifa tuzitakazo sisi wenyewe. Sifa alizoweka Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) za kuchaguana ni:

 

1.     Kuchaguana kwa msingi wa Dini, sio nasaba, rangi, mali au urembo.

2.     Msingi wa maadili mema na tabia nzuri.

3.     Mahusiano na maingiliano mema.

 

Hayo yanaweza kujulikana tu kwa kumchunguza aliyekuja kuposa kwa misingi ya Uislamu na kufikia muafaka na ufumbuzi aina fulani. Kama ungefanya hivyo basi ungejua hali ya mumeo kabla ya kuingia katika Nikaah hiyo. Ama kwa kuwa shida hiyo tayari ipo na unaishi nayo tunaona unaweza kutumia mbinu zifuatazo kuliondoa tatizo hilo:

 

1.     Anza mwanzo kuzungumza naye kwa njia nzuri kuhusu hilo wakati ambao utaona mnasibu kwake yeye kukusikiliza. Itabidi usome suala hili kwa kina ili uweze kumueleza kwa njia ambayo atakufahamu. Allaah Aliyetukuka Anasema:

ادْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ ۖ 

Lingania katika njia ya Rabb wako kwa hikmah na mawaidha mazuri. [An-Nahl: 125]

 

2.     Jaribu kumshawishi awe ni mwenye kwenda kuswali na kusikiliza mawaidha katika Msikiti wa Sunnah.

3.   Ikishindikana tumia watu ambao ni rafiki zake wa karibu wenye msimamo kama wako wazungumze naye.

4.     Jaribu kupata makala, vitabu, kaseti kuhusu kadhiya hiyo umpatie asome au asikilize.

5.    Muombe Allaah Aliyetukuka sana baada ya Swaalah, wakati umefunga, unapoinuka usiku kwa ajili ya Tahajjud na nyakati ambamo du’aa hukubaliwa ili umuombee aongozwe.

 

Hali kadhalika soma makala zifuatazo ili upate hoja za kumkinaisha kuachana na mambo hayo, au unaweza kumchapishia yeye azisome.

 

Hukumu Ya Kusherehekea Kuzaliwa Kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam)

 

Sababu 21 Za Kumfanya Muislam Asisherehekee Maulidi

 

Mawlid – Historia Yake, Hukmu Na Kauli Za Maulamaa

 

Makosa Yaliyomo Katika Mawlid Ya Barzanjiy, Burdaa, Nuwn, Sumtudurrar, Dalaailul Khayraat, Du'aa Ya Wasiylah Na Mawlid Mengine 

 

Mawlid Ni Bid'ah Na Vigawanyo Vya Bid'ah Pia Ni Bid'ah

 

Jinsi Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam) Alivyokuwa Akisherehekea Mazazi Yake

 

Mawlid (Kusherehekea Kuzaliwa Kwa Mtume)

 

Kila Uzushi Ni Upotofu, Hata Kama Watu Watauona Kuwa Ni Mzuri

 

Vizuizi 12 Dhidi Ya Kusherehekea Kuzaliwa Kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)

 

 

Tunakutakia mafanikio mema katika hilo.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share