Hupata Damu Baada Ya Kujimai Na Mume – Vipi Kujitibu Na Majini Wa Mahaba?

SWALI:

 

Assalam alaykum jamiaan. Bismilah Rahman Rahim,

 
Nina wingi wa heshima kutoa shukurani zangu kwenu na kwa waislamu wote kwa jumla kwa kutuelimsha na kutueka sawa katika mambo tofauti yanayotupa utata. Mimi ni mwana ndoa, naomba kupatiwa ufumbuzi wa Dua au Visomo vya Ruqya kwa ajili ya kujikinga na majini mahaba ambao wananitatiza sana mimi na mume wangu, mara nyingi huwa natokewa na damu wakati wa kujaamiiiana na mume wangu, nilifika vituo vya afya na kufanya uchunguzi wa njia zangu za uzazi na bahati nzuri alhamdullillah nikaonekana sina tatizo lakini cha kushangaza ni kwamba ikisita damu kama nikiwa mkavu basi sipati raha ya tendo na mume wangu huwa anamaliza mapema sana. Nina mwaka na miezi nane lakini hata siku moja sijaona furaha ya tendo.

 
Naomba munipe ushauri ili nami nifurahie tendo hilo.


Wabillah tawfiq

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako.

 

Muislamu anatakiwa ajikinge kila wakati kwa kinga ambazo tumeelezewa na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ikiwa ni ya Shaytwaani, hasadi na maafa mengine yanayotokana na hayo.

 

Kinga inatakiwa ichukuliwe kabla ya kukumbwa na janga hilo lakini pia ikiwa tayari umeathirika inabidi ujtibu kwa njia zilizo sahihi. Kwa sasa tunakushauri ufanye mambo mawili ambayo ni muhimu:

 

Jambo la kwanza ni kuanza kusoma Aayah au Surah za Qur-aan zinazohusiana na suala hilo lako. Na katika hilo visomo ni kama vifuatavyo:

 

Kusoma Aayah kumi za al-Baqarah (2) ambazo zinaepusha nyumba zetu na Mashaytwaan. Nazo ni kuanzia Ayah 1-5, 255-257 na 284-286. Hizi Aayah zinatakiwa zisomwe asubuhi na jioni.

 

Kusoma Suratul Ikhlaasw, al-Falaq na an-Naas mara tatu tatu, asubuhi na jioni na pia wakati wa kulala.

 

 

Na Qur-aan yote ni dawa inatakiwa kila Muislamu awe na ada ya kuisoma na kujua maana yake na kutekeleza yaliyomo ndani yake.

 

 

Usome du’aa ambazo ni kinga unapotoka nyumbani na unapoingia.

 

 

Du’aa ambayo wewe na mumeo mnatakiwa msome wakati wa kitendo cha ndoa ambayo inawalinda na kukilinda kitoto kitakachoingia na Shaytwaan.

 

 

Adhkaar za baada ya Swalah na pia wakati wa kulala.

 

 

Usome adhkaar za asubuhi na jioni.

 

 

Adhkaar nyingine ni kama, BismiLlaahi Arqiyk min kulli shay-in yu’dhiyka wa min sharri kulli nafsin aw ‘aynin haasidin. Allaahu yashfiyk BismLllaahi arqiyk (Muslim, at-Tirmidhiy, an-Nasaa’iy na Ibn Maajah). Kwa du’aa hii mume atamsomea mkewe na kinyume chake. Na du’aa nyingine ya kusomeana mara tatu ni, BismiLlaahi arqiyk WaLlaahi yashfiyk min kulli daa’in fiyk wa min kulli an-Naffaathaati fil ‘uqad wa min sharri haasidin idhaa hasad(al-Haakim na Ibn Abi Shaybah). Na pia, U‘idhuka bikalimaatiLlaahi at-Taamaati min kuli Shaytwaanin wa haamah wa min kulli ‘aynin laamah (al-Bukhaariy).

 

Na hizi adhkaar pamoja na nyingine unaweza kuzipata katika kijitabu ambacho ni muhimu sana nacho ni Hiswn al-Muslim (Kinga ya Muislamu), kinachopatikana hapa:

 

Hiswnul Muslim

 

Pia bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi yam as-ala haya:

 

 Naingiliwa Na Majini

 

Kuhusu Mashaytwaan Na Vipi Kujikinga Nao

 

Anapoweweseka Usiku Asomewe Surah Gani?

 

 

Nimeambiwa Nina Jini La Kiislamu Kwa Sababu Ya Kupenda Sana Dini

 

Mke Wangu Amevaliwa Na Majini Wa Mahaba? Hapendi Kutenda Kitendo Cha Ndoa Na Mimi

 

 

 

Jambo la pili, ni wewe na mume wako kwenda kwa Shaykh aliye mjuzi wa mas-ala ya Ruqyah ya kisheria, ambaye ni mchaji Mungu aweze kuwasomea kwa njia ya Kishari’ah na InshaAllaah mtapona na ugonjwa wenu huo.

 

Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Awapatie shifaa ya haraka.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share