Maiti Aliyekufa Zaidi Ya Wiki, Hajulikani Kafa Kwa Nini, Anahitaji Kuswaliwa?

 

Maiti Aliyekufa Zaidi Ya Wiki, Hajulikani Kafa Kwa Nini, Anahitaji Kuswaliwa?

 

Alhidaaya.com

 

Swali:

 

Assalam alaykum! Sheria yaniamrisha vipi! Ikiwa ntaletewa habari kuna maiti yako chumba cha kuhifadhia maiti. Nilipoenda amekufa kama wiki hivi na hakuna uhakika amekufa na nini jee ni mswalie ama nimzike tu?

 

 

Jibu:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Maiti yeyote anayepatikana hata ikipita muda anatakiwa afanyiwe mambo manne kisheria isipokuwa ikiwa labda ameoza kabisa na mengine hayawezi kufanyika.

 

Mambo yenyewe ni:

 

1.     Kuoshwa inavyofaa kisheria.

2.     Kukafiniwa (kuvikwa sanda).

3.     Kuswaliwa, na

4.     Kuzikwa.

 

Na huyo maiti kwa kuwa alikuwa katika chumba cha kuhifadhiwa maiti atakuwa yuko katika hali nzuri, hivyo anatakiwa afanyiwe mambo yote hayo manne. Ikiwa itahitajika kikanuni awe ajulikane amekufa kwa sababu ipi anaweza kucheleweshwa kuzikwa ili afanyiwe uchunguzi. Na uchunguzi huo ukimalizika tu afanyiwe yanayopaswa kufanyiwa kisheria.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share