Swalah Za Uzushi KuhusuTahajjud Na Usiku Wa Ijumaa

 

Swalah Za Uzushi KuhusuTahajjud Na Usiku Wa Ijumaa

 

Alhidaaya.com

 

 

Swali La Kwanza:

 

 

Asslaamualykum   Ndugu Zangu,

 

Naomba Kuwa Uliza   Nisaidieni,

 

Nimepewa    Kartasi  Iliyiandikwa   Sunna Za Kila Siku

 

Usiku---yaani   Kuzisali   Ta Fauti Mfano:  Usiku Wa Alkhamis -  Wakuamkia Ijumaa  Sali Rakaa 2  Kila Rakaa   Baada Ya Surah Fatiha  Soma  Surah Izazulzila Mara  15 Baada Salaam   Soma  Yahayyu Ya Kayyum

 

Yazuljalaliwalikraam Mara  100

 

Plz Put Light On This Issue.   Nawaomba  Samahani   Kama Nimewa Kosa

 

Jazaakallahukheir      Fiamaanillah

 

 

Swali La Pili:

 

Asalam alykum warahmatulahi wabarakatu  nimekuwa natakuwauliza kuhusu swala za usiku ama gisi nime soma wanasema kama mtu unasoma sura elfu moja ao miya unapata swawabu nyingi. sasa kama mtu ajuwi izo sura zote unajuwa tu tano ao kumi uta fanya aje?

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Hakuna Swalaah za Sunnah hasa za usiku isipokuwa ni Sunnah ya Tahajjud, nazo ni kuswali Rakaa mbili au nne, au sita, au nane na kumalizia na Rakaa tatu za Witr.

 

Wala hakuna Swalah hasa ya usiku wa Alkhamiys kuamkia Ijumaa au siku yoyote katika wiki. Na kusoma Suwrah hizo au kutaja majina ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) pia hakuna dalili yoyote iliyokuja kutufundisha kuzisoma Suwrah hizo na majina kwa idadi yoyote.

 

 

Uzushi mwingi wa ibada unazushwa na wengi wasiojua ambao hufuata bila ya kuchunguza kwanza wala kuwa na elimu sahihi. Mara nyingi ibada hizo hutaja idadi kubwa ya kusoma Suwrah au dhikr fulani kama kutaja majina ya Allaah, au tasbiyh kama alivyouliza muulizaji wa Swali la pili.

 

 

Uzushi unafika kusema 'soma Suwrah Al-Baqarah mara tatu' au 'soma Suwrah Yaasiyn mara nne' au 'soma Qul-Huwa Allahu Ahad mara elfu'. Uko wapi huo muda wa mtu kukaa kusoma suwrah zote hizo? Hatuoni kuwa huku ni kujitia mashaka tu ya kufanya ibada ngumu kama hizi ambazo hazina thamani yoyote? Ibada zetu zilizothibiti ni nyepesi kabisa, lakini watu wamezifanya ni ngumu kwa kuzua uzushi mwingi kama huu.

 

 

Nasiha yetu ni kwamba kabla ya kufanya ibada yoyote ni vizuri kuhakikisha kama ni sahihi. Kisha tumia wakati wako huo kufanya ibada ambazo hazina shaka kabisa na hakika zitakupatia thawabu. Kama hizi zifuatazo:

 

1.    Kusoma Qur-aan na kujitahidi kukhitimisha kwa mwezi mara moja au zaidi ya hivyo. Kila herufi utakayosoma katika Qur-aan ni thawabu mara kumi.

 

2.    Soma tafsiri ya Qur-aan upate kujua maana ya maneno ya Rabb wako, nayo ina fadhila kubwa kufahamu Qur-aan.

 

3.    Anza kuhifadhi Qur-aan ikusaidie katika Swalah yako, na pia kuhifadhi Qur-aan kuna fadhilia kubwa kwani siku ya Qiyaama utapandishwa daraja ya Pepo kwa kila Aayah uliyoihifadhi.

 

4.    Fanya adhkaar zilizothibitika ambazo zote utazipata katika kitabu cha 'Hiswnul-Muslim' kinachopatikana katika kiungo kifuatacho humu Alhidaaya.com:

 

 

Hiswnul-Muslim: Du’aa Na Adhkaar Kusoma Na Kwa Kusikiliza (Toleo Lilohaririwa)

 

5.    Sikiliza mawaidha ambayo ni njia bora kabisa ya kukuongezea elimu yako na pia kuzidisha imani yako ya dini.

 

6.    Soma vitabu vya dini, kama vya Hadiyth za Nabiy (Swalla Allahu 'alayhi wa   aalihi wa sallam), na vitabu vingi vya dini vimejaa. Hii ni kuongeza elimu ya dini yako ambayo pia ina fadhila kubwa.

 

Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Atuzindue na kila uzushi na yote yaliyo batili na Atuonyeshe yaliyo haki na Atuwezeshe kuyafuata.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

 

Share