Hawajafanya Jimai Bali Wamefanya Matendo Mengine Wanahesabiwa Wamezini? Nini Hukmu Yao?

 

SWALI:

 

ASSALAMU ALAYKUM, NINATAKA UFAFANUZI KUZINI NI KULE KWA MWANAMME KUUINGIZA UTUPU WAKE KWA MWANAMKE AU HATA KAMA HAJAUINGIZA TAYARI WANAKUWA WAMESHAZINI. NA JEE KAMA WATATUBIA KWA KOSA LA KUFANYA HILO TENDO BILA YA TUPU YA MWANAMME KUINGIA KWENYE TUPU YA MWANAMKE NI LAZIMA IPITISHWE ILE HUKUMU YA ALLAH SUBHANAHU WATAALA YA KUPIGWA MAWE AU MIKWAJU MIA?

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu hukumu kwa mwanamme na mwanamke kufanya starehe bila ya kuzini hasa.

Hakika ni kuwa katika Uislamu zinaa inayochukuliwa kuwa ni ile halisi ni kule kujamiiana mwanamme na mwanamke ambao si wanandoa kishari’ah. Hao ndio wenye kupata adhabu ya kishari’ah – ikiwa hajaoa au kuolewa basi adhabu yake ni kupigwa mikwaju mia na ikiwa ameoa au kuolewa, yuko katika ndoa au ametalikiwa basi adhabu ni kupigwa mawe hadi kufa. Kwa ufupi zinaa ni kuingia utupu wa mwanamme kwenye utupu wa mwanamke.

 

Mbali na kitendo hicho cha kuthibitisha jimai vitendo vingine vinahesabiwa kuwa ni zinaa lakini hakuna adhabu kwa mwenye kufanya ila tu anapata madhambi na anahitajika kuomba tawbah kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala).

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) huku Anawakataza waja Wake wasizini na kuikaribia na kuchanganyika na sababu zitakazo kupelekea katika uzinzi. Anasema Aliyetukuka:

Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu” (al-Israa’ [17]: 32), yaani ni dhambi kubwa.

Na pia, “Na ni njia mbaya”, yaani ni njia mbaya sana kwa mtu kuifuata. Kila kiungo katika mwili wa mwanaadamu kinazini kama alivyotuelezea Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam), mikono, miguu, mdomo, macho na viungo vinginevyo.

 

Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:

 

Kufanya Mapenzi Bila Ya Kitendo Cha Ndoa Kwa Ambaye Hajaolewa?

 

 

Kulala Pamoja Bila Ya Kufunga Ndoa

 

Nakaribia Kuzini na Mke wa Ndugu Yangu Vipi Nijiokoe?

 

Nakaribia Kuzini Na Shemeji, Je, Nifanyeje Kujiepusha Na Vipi Nitahukumiwa Na Allaah?

 

 

Ikiwa mtu amefanya mambo mengine bila ya kujimai kabisa inatakiwa afuate na kutekeleza masharti yafuatayo ili aweze kusamehewa na Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):

 

1.     Asirudie tena kosa hilo.

2.     Ajute kwa kufanya kosa hilo.

3.     Aweke azma ya kutorudia tena.

 

Ukiwa mtu atatekeleza masharti hayo basi Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Atamsamehe.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share