Sandwichi Ya Mchicha Na Jibini

Sandwichi Ya Mchicha Na Jibini

Vipimo

Mkate - 1 mrefu

*Sosi ya pizza au makaroni

Chumvi - kiasi

Pilipili  manga - kiasi

Jibini (cheese) - ½ kilo iliyochunwa

Kitunguu - ½ kikate slice

Nyanya - 1 ikate slice

Zaituni (olives) - 5 zikate slice

Mchicha mchanga - ½ kikombe cha chai

Uyoga - ½ kikombe zilizokatwa slice

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Anza kuwasha oveni moto wa 350°F.
  2. Kata mkate wako katikati juu na chini.
  3. Halafu pakaza sosi yako ya makoroni kiasi kwenye kipande cha chini cha mkate (usitie nyingi mkate utanywea)K
  4. isha nyunyizia cheese kiasi halafu vipange vitu vyote ulivyokata slice ukianza na mchicha, uyoga,zaituni vitunguu, nyanya,  chumvi na pilipili manga halafu malizia na cheese iliyobaki.
  5. Kisha tia kwenye oven kwa muda wa dakika 10-15 na kipande cha juu cha mkate kichome pembeni kwa muda wa dakika 3-5.
  6. Ukisha kuwa tayari toa na funika kipande cha juu cha mkate tayari kwa kuliwa.

Kidokezo:

*Tazama kwenye macaroni ya nyama ya kusaga na bashameli namna ya  kutengeneza au nunua ya kopo iliyo tayari. Ikibidi unaweza kutumia nyanya ya kopo badala ya sosi ya macaroni

 

Share