Alhidaaya Wanayo Madrasa Afrika Mashariki Ili Awapeleke Wanawe Wapate Mafunzo Swahiyh?

SWALI:

 

Alhamdullillah Namshukuru Mungu kwa kuwaezesha kutuelimisha. Napenda kuwaluliza je muna madrassa ama shule Kenya ama Tanzania. Ingekuwa vizuri kwa watoto wetu kupata elimu ya dunia na dini kwenye shule zetu za kiislamu khusasan ahli sunna kama nyinyi. Nia yangu kama muna shule ingekuwa vizuri saana ili watoto wetu wapate elimu ya dunia na ya dini yao. Na kama hamna basi nawaombea Mungu Awawezeshe mufungue ili tupate mustaqbal mwema kwa watoto wetu.

 

Wasalam Aleikum.

 

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu Alhidaaya kuwa na Madrassah Afrika Mashariki.

 

Hakika Alhidaaya haina Madrassah yoyote ile inayoiendesha ila wahusika wake wanafanya harakati mbalimbali za kida’wah kama ufundishaji na usimamizi wa masuala ya dini.

 

Alhidaaya inahusika na tovuti hii tu iliyo mbele yako.

 

Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Atuwezeshe kufanya mengi zaidi kama uliyoyaulizia na mengine ya kuisimamia na kuihudumia dini hii adhimu.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share