Anapata Upungufu Wa Nguvu Kila Akijimai Na Mkewe Afanyeje Ili Aimarishe Ndoa Yake?

SWALI:

 

asalam alakoum.,

mimi nataka munijulishe vipi ntapata matibabu ya mwili wangu. Mimi kila mara nikikutana na mke wengu kimapenzi nguvu zina pungua. Sijuwi kwa nini. Munipe owongozi ili ni pate dawa ndoa yangu isivunjike.

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kukosa nguvu za kiume.

Hakika hili ni tatizo ambalo huwakumba baadhi ya wanaume au hata wanawake, kukosa nguvu za kuweza kustarehe na mwendani katika ndoa.

 

Tatizo hilo hutokea kwa kupatikana na ugonjwa au kutopata lishe bora au kutojua kuendeleza kitendo cha jimai. Ushauri ambao tunaweza kukupatia ni mwanzo uende kwa madaktari waliobobea katika mas-ala ya uzazi ili wafanye uchunguzi na waje katika matibabu. Pia unaweza kwenda kwa matwabibu wanaotumia madawa ya Ki-Sunnah kwa wajuzi kuhusu utabibu wa aina hiyo. Na kwa uwezo wa Allaah Aliyetukuka utatulia.

 

Njia nyingine ni kupata lishe bora ambazo zinaongeza nguvu za kimwili kwa mwanaadamu. Hili pia unaweza kuwaona wataalamu wajuzi wa lishe ambao watakupatia nasaha kemkemu kuhusu hilo. Na njia nyingine ni kutokufanya haraka katika kufanya kitendo cha jimai. Unatakiwa uanze na vitangulizi vya jimai ili kuhifadhi hiyo nguvu ambayo ni pungufu. Inatakiwa uanze kwa mazungumzo yaliyo matamu na mkeo, umshike shike na kumpiga busu mpaka unapojihisi kuwa sasa uko tayari ndio ufanye jimai. Kwa kufanya hayo tunatarajia kuwa mambo yatakuwa sawa.

 

Hakuna ugonjwa wa aina yoyote ila una dawa yake. Na InshaAllaah Allaah Aliyetukuka Atakuafu kwa hayo uliyo nayo.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share