Kushadidia Jambo Bila Masharti Ya Ushahidi Wa Kishari’ah

SWALI:

 

Assalam aleykum warahmatullah wabarakatuh.

Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa uongozi mzima wa Alhidaaya kwa mafunzo mema wanayotupatia. Inshallah mungu atawalipa leo duniani na kesho akhera.

 

Nini hukmu ya mtu mwenye dini kushadidia jambo na kuapa kuwa jambo fulani limefanyika kutokana tu na mazingira fulani na si kama dini inavyosema wapatikane mashahidi watatu?

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kushadidia jambo na kuapa katika hilo. Haifai kwa mtu na hasa aliye na Dini kama unavyomuita kushadidia jambo kwani Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Wameangamia wenye kuchupa mipaka”. Na akalikariri hilo mara tatu.” (al-Bukhaariy).

 

Dini hii ni Dini ya dalili na mtu kukubali dalili na hoja za sawa pindi zinapomfikia bila kukazania kufuata na kushadidia ya kwake. Hivyo, ni muhimu mtu anashikamana na yale yaliyothibiti katika shari’ah na si kuyafuata yale ambayo hisia zake humtuma japokuwa anaziamini sana hisia zake na japokuwa hisia zake zinamili katika ukweli kutokana na mazingira anayoyafahamu yeye au aliyoyazoea.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share