Aliritadi Kisha Akarejea Katika Diyn, Je, Kuna Analopaswa Kulifanya Ili Asameheke?

 

SWALI:

asalam aleikum

nina dadaangu katika dini miaka miwili iliopita alipata ufuasi mbaya akaingia kuwa mkristo ingawa yeye kazaliwa uislamuni lakini miezi sita iliopita aliamua kurudi tena uislamuni na kutaka msamaha kwa ALLAH je atakiwa kutenda lolote msamaha wake ukubalike kidini na je atende nini kusafisha moyo wake na kujua kweli amesameheka

 


JIBU:

 

Sifa zote njema zamstahikia Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Rehma na amani zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Kutoka katika Dini -kurtad- si jambo jepesi na likitokea huwa linawatokezea wale ambao toka mwanzo hawakuwa Waislamu wa kweli kweli; na dada yako huyu alitoka na sasa amerudi lakini kilichomtoa na kumrudisha ni nini? Pengine wasi wasi kuwa mumemtenga au atakosa manufaa fulani kutoka familia na kadhalika; kwani kama kweli alikuwa Muislamu basi hakuna sababu yoyote ile ya kumtoa katika Uislamu hasa hasa ukiangalia ni dini ipi aliingia baada ya kutoka Uislamu; kwani zote zinaabudu viumbe na matamanio yao.

Cha kufanya ni dada yako kutafuta elimu sahihi ya dini yake na huko ndiko kusafisha moyo wake, kisha arudi kwa Mola wake kwa kuomba tawbah ya kweli na kuhakikisha kuwa kila wakati anajuta kwa alichokifanya kila akikumbuka na kila akipita sehemu alizokuwa akienda kumshirikisha Allaah na kuwa na Iymaan kuwa Allaah Atamkubali na kutenda mema kwa wingi.

Pia kumshukuru Allaah kuwa ameweza kurudi katika Dini sahihi; Dini Anayoiridhia Allaah kabla hajaaga dunia, kwani kama angelikufa hali ni kafiri basi Qur-aan inamwambia hivi:

Wala hawatoacha kupigana nanyi mpaka wakutoeni katika Dini yenu kama wakiweza. Na yeyote katika nyinyi akiacha Dini yake akafa naye ni kafiri, basi hao ndio ambao ‘amali zao zimeharibika duniani na Akhera. Na hao ndio watu wa Motoni; humo watadumu.” Al-Baqarah: 217

 

Na Alalah Anajua zaidi

 

 

 

Share