Mume Kumwambia Mkewe Kuwa Akistarehe Naye Ndio Talaka Sasa Anajuta Kwani Anamtaka Mkewe Afanyeje?

SWALI:

 

Assalam alaykum - wallah ninasuala gumu kwangu. Na suala lenyewe ni hili mimi mume nimemtamkia mke wangu kwamba nikitembea nae kimwili ndo talaka yake wallah ninajuta kusema hivyo na bado nina muhitaji mke wangu lakini nifanyaje ili niondoshe ili niwe safi kwa mke wangu kiislam.

 


 

 

JIBU

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mume kumwambia mkewe nikistarehe nawe ndio talaka. Hiyo ni talaka iliyowekewa sharti. Kwa hiyo, pindi utakapo starehe na mkeo talaka itakuwa imepita, kwani talaka ni suala ambalo halina mzaha kabisa.

 

Kwa ajili hiyo, una njia mbili ambazo unaweza kufuata ili kutatua au kuzidisha tatizo hilo.

 

  1. Ni wewe kustarehe naye. Ukistarehe tu naye itakuwa umemtaliki mke wako. Ikiwa hiyo ni talaka ya kwanza au ya pili utakuwa na fursa ya kumrudia tena kabla ya eda kumalizika.

 

  1. Ni kukaa naye bila ya kustarehe naye ili talaka isipite. Hata hivyo, njia hii ya pili ina tatizo, moja ni kuwa wewe hutaweza kuvumilia na pia mke wako. Hali ikiwa hivyo, mke anaweza kudai talaka kupitia kwa Qadhi kwa sababu humpatii haki yake ya kimwili.

 

Kwa njia yoyote utakayo tumia, tunakunasihi kama ndugu yetu usiwe ni mwenye kufanya mzaha na talaka, kwani hata ukiisema kwa mzaha inakuwa ni yenye kuhesabiwa na kupita.

 

Bonyeza viungo vifutavyo upate maelezo zaidi:

 

Mume Kutamka 'Kila Mtu Ajue Maisha Yake' Ina Maana Ni Talaka?

 

Mume Kamtamkia Mkewe Talaka Kisha Akataka Kumrejea Katika Eda, Mwanamke Anayo Haki Kukataa Kurudiana Na Mumewe?

 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi.

 

Share