Ikiwa Mume Hajamgusa Mkewe Muda Wa Miezi Mitatu Ina Maana Kuwa Keshamtaliki?

SWALI:

 

Asalam aleikum warahma tullahi wabarakatu.

Nawashukuru kwa kila njiya si kwa kidini wala duniya nawaombeya dua'a kwa kila swala mafanikio inshallah.nawaomba ndugi zanguni munijibu suala langu hili, kama bwana hajamgusa mkewe kwa muda mwezi au miyezi mitatu! Jee yamanishe ameshampa talaka? Shukan jazaki allahu kheir.

 

Asalam aleikum warahma tuallahi wabarakatu.

nawamba nduguzanguni kwa uwezo wa allah munijibu kwa haraka, na suala langu ni hili kama mume yuko mjini lakini hamgusi mkewe kwa miyezi 3 au zaidi na niya yake huwa ni kumuata lakini hakutamka!! Jee yamanisha ashamuata huyo mke? Shukran wajazaka allahu kheir.

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kuwepo kwa mume mjini na asimguze kwa maana ya kustarehe naye kwa muda wa mwezi au miezi mitatu. Ikiwa hali ni hiyo sio tu miezi mitatu, bali hata ikiwa zaidi ya miezi mitatu mume hajamgusa mkewe, mke anakuwa bado ni mke wa mtu mpaka apatiwe talaka ima ya kwa mdomo au kwa maandishi.

 

Hata hivyo, kukaa miezi yote hiyo si kawaida kwa wanandoa kwa ajili hiyo inabidi kwa mke ajaribu mbinu za uke wake wa kumchokoza mumewe ili waweze kustarehe. Mke ana haki ya kustareheshwa na mumewe na kutostareheshwa huko ni sababu moja ya mke kudai talaka na kujitoa katika ndoa. Inatakiwa mume na mke wapatiwe ushauri nasaha kuhusu mas-ala yanayohusiana na ndoa.

 

Labda sisi tukiuliza ni kuwa kuanzia mume aoe hajamgusa mkewe au vipi? Ikiwa katika mke kuzungumza na mumewe au kupata ushauri nasaha na hakuna natija yoyote iliyopatikana, itabidi kuitishwe kikao kuzungumzia tatizo hilo baina yako wewe, mumeo, wazazi wako na wake au wawakilishi wenu kuhusu suala hilo.

 

Tuna matumaini makubwa sana kuwa kwa kufanya hivyo kutapatikana ufumbuzi muruwa kabisa.

 

 

 

Mume Kahama Chumba Kwa Miezi 3 Hafanyi Tendo La Ndoa, Akiulizwa Anasema Anachoka Kazini

 

 

 

Talaka Ikiwa mume Yuko Mbali Na Mke Muda Mrefu

 

Je, Inafaa Mume Na Mke Kuishi Mbali Kwa Muda Mrefu?

 

Nimeoa Mwezi Wa Pili Lakini Mke Hataki Kuingia Katika Kitendo Cha Ndoa

 

 

Na Allaah Anajua zaidi.

 

 

Share