Kumtamkia Mke Talaka Kisha Kutaka Kumrudia

SWALI:

 

A/a mume wamgu alinitamkiya kuwa nimekuwacha baada muda mchache ananitamkiya nimekurejea. jee hii talaka inasihi au haisihi?


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mumeo kukuacha na kisha kukurudia.

Ama hakika kuacha (yaani kumuacha mke) na kumrudia ni mambo ambayo hayana mzaha. Hiyo ina maana ukisema umemuacha huwa ameachika na ukisema umemrudia inakuwa tayari umemrudia kwa kutumia masharti yaliyowekwa na shari’ah.

 

Mwanzo hiyo talaka aliyokupa mumeo imepita, ila mumeo atakuwa ana dhambi ikiwa amekuacha ukiwa katika hedhi au twahara ambayo amekuingilia (amefanya jimai na wewe).

Ama kukurudia itakuwa sawa ikiwa atafanya hivyo kabla ya eda yako kumalizika, yaani kabla ya kumalizika hedhi zako tatu. Hata hivyo, hawezi kukurudia tena ikiwa hiyo ni talaka ya tatu mpaka uolewe na mume mwengine kisha akuache baada ya kustarehe nawe. Na pia hawezi kukurudia bila ya Nikaah ikiwa umemaliza eda yako. Ikiwa eda yako imemalizika naye anataka kukurudia basi itabidi akupose upya, ukubali, kuwe na Nikaah mpya pamoja na kulipwa mahari utakayo.

 

Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:

 

Mume Kamtamkia Mkewe Talaka Kisha Akataka Kumrejea Katika Eda, Mwanamke Anayo Haki Kukataa Kurudiana Na Mumewe?

Mas-ala Ya Talaka Mbali Mbali

Talaka Ziko Aina Ngapi Na Wakati Gani Zinasihi?

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share