Mashia (Maraafidhah) Na Uharibifu Wa Qur-aan

 

 Mashia (Maraafidhah) Na Uharibifu Wa Qur-aan

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Nimewahi pia kusikia kutoka kwa rafiki yangu wa Kishia kwamba kuna surah ndani ya kitabu chao ambayo haimo ndani ya Qur-aan. Unaweza kuthibitisha vipi kuhusu hili? Surah wenyewe ndani ya kitabu chao inaitwa Suratul-Wilaayah.

Shukrani zote zinamstahikia Allaah.

 

Kwa mnasaba wa Suratul-Wilaayah, baadhi ya wanachuoni wa Kishia na Maimamu wao wamesema kwamba (hiyo surah) ipo. Yeyote miongoni mwao anayekana basi anafanya hivyo kwa mfumo wa taqiyah (unafiki). Miongoni mwa aliyeeleza wazi wazi kwamba ipo ni Mirza Husayn Muhammad Taqiyun-Nuuri at-Tubruusi (amefariki 1320 AH). Ameandika kitabu ambacho anadai kwamba Qur-aan imeharibiwa na kwamba Maswahaabah wameficha baadhi ya sehemu zake (Qur-aan), ikiwemo Suratul-Wilaayah.

 

Baada ya kifo chake, Maaraafidhah walimpatia heshima kwa kumzika sehemu za an-Najaf. Kitabu hichi kilichoandikwa na at-Tubruusi kilichapishwa nchini Iran mwaka 1298 AH, na baada ya chapisho hilo kulikuwa na msongamano mkubwa kwa sababu walitaka kuuona upungufu wa Qur-aan, ambao hapo kabla ulikuwa ukijulikana na viongozi wao tu, uliendelea kubaki kwenye vyanzo mbalimbali ndani ya mamia mwa vitabu vyao vikuu. Mwanzoni mwa kitabu chake amesema:

 

“Hichi ni kitabu kizuri na kinachoheshimika chenye jina la Faslul-Khitaab fi ithbaat tahriyf Kitaab Rabbil-Arbaab (Maelezo muhimu kuhusiana na uharibifu wa Kitabu cha Bwana wa Mabwana)... Ametaja Aayah na surah ambazo anadai kwamba Maswahaabah wamezificha, ikiwemo Suratul-Wilaayah.” Maandiko ambayo, kwa mujibu wa maelezo yao, na kama vile yanavyonukuliwa ndani ya kitabu hichi, ni:

 

“Enyi mlioamini, muaminini Mtume na Walii [yaani ‘Aliy] ambaye sisi tumewaleta kuwaongoza nyinyi katika njia sahihi, Mtume na Walii ambao kila mmoja ni sehemu ya mwenziwe, na Mimi ni Mwenye elimu zote, Yote yanatambulikana...” 

 

Halikadhalika wana surah nyengine wanayoiita Suratun-Nuurayn:

 

“Enyi mlioamini, aminini kwenye nuru mbili (an-Nuurayn) ambazo tumeziteremesha kwenu ili muzisome Ayah zangu na kuwaonya kuhusu adhabu ya Siku kubwa. Hizo ni sehemu [moja] kwa mwenziwe na Mimi ni Mwenye elimu zote, Yote yanatambulikana. Wale ambao wanatekeleza ahadi pamoja na Allaah na Mtume Wake kama yalivyoelezwa ndani ya ayah (za Qur-aan), Mabustani ya starehe yatakuwa ni yao, lakini wale wasioamini baada ya kuamini kwa kuvunja ahadi zao na kutotii amri za Mtume, watatupwa Motoni. Wamejitia kwenye makosa na kwenda kinyume na wasiyyah wa Mtume (yaani uteuzi wa ‘Aliy kama ni Khaliyfah), na watapewa kinywaji cha maji ya moto...”

Na maelezo mengine ya kipuuzi.

 

Unaweza kuipata surah kamili chini kabisa ya makala hii pamoja na picha ya surah hiyo kutoka katika msahafu wa Kifursi*

 

 

Prof. Muhammad ‘Aliy as-Su’uudi – ambaye aliwahi kuwa ni mtaalamu mkubwa wa Wizara ya Sheria nchini Misri – amefanyia utafiti wa msahafu wa Kiirani uliokuwa mikononi mwa Bw. Bryan mwenye elimu ya lugha na historia katika nchi za mashariki, ambaye alifanikiwa kupata nakala ya ya surah hii; juu ya mistari ya maandishi ya Kiarabu kuna maandishi ya tafsiri kwa lugha ya Kiirani.

 

Kama ilivyoelezwa na at-Tubruusi ndani ya kitabu chake, Faslul-Khitaab fi ithbaat tahriyf Kitaab Rabbil-Arbaab, pia inaelezwa ndani ya vitabu vyao Dabastan Madhaahib, ambacho kipo kwa lugha ya Kifursi, kilichoandikwa na Muhsin Faani al-Kashmiri. Kitabu hichi kimechapishwa mara kadhaa nchini Iran, na surah hii ya uongo ilinukuliwa ndani ya kitabu cha Historia ya Maandiko ya Qur-aan, The History of Qur-anic Manuscripts, 2/120 kilichoandikwa na Bw. Noeldeke mwenye elimu ya lugha na historia katika nchi za mashariki, kitabu ambacho kimechapishwa na gazeti la Kifaransa na Kiasia French Asian newspaper mwaka 1842 (uk. 431-439).

 

Pia imeelezwa na Mirza Habibullaah al-Haashimiy al-Khuu’i ndani ya kitabu chake cha Manhaaj al-Baraa’ah fi Sharh Nahj al-Balaaghah (2/217); na Muhammad Baaqir al-Majlisi ndani ya kitabu chake cha Tadhkiratul-A’immah (uk. 19, 20) katika lugha ya Kifursi, (kimechapishwa na) Manshuurah Mawlana, Iran.

 

Pia angalia al-Khutuut al-‘Ariydhah li’l-Asas allati qaama ‘alayha diin ash-Shi’ah cha Muhiibud-Diyn al-Khatwiyb.

 

Madai yao haya ni kukana maneno ya Allaah (tafsiri ya maana):

 

 

إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ ﴿٩﴾

Hakika Sisi Tumeteremsha Adh-Dhikra (Qur-aan) na hakika Sisi bila shaka ndio Wenye kuihifadhi. [Al-Hijr 15: 9].

 

 

 

Hivyo Waislamu bila ya utata wowote wamekubaliana kwamba yeyote anayedai kwamba kitu chochote ndani ya Qur-aani kimegeuzwa au kimebadilishwa basi ni kafiri.

 

Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

 

“[Hukumu hiyo] Pia inatumika kwa wale ambao wanaodai kwamba baadhi ya Aayah za Qur-aan zimetolewa au kufichwa, au wanaodai kuwa wana tafsiri tofauti na za maajabu, madai ambayo yanawazuia kutekeleza maamrisho kama yalivyoelezwa ndani ya Shari’ah n.k., ambao wanaitwa al-Qaraamitah na al-Baatwiniyyah, na wenye kujumuisha at-Tanaasukhiyyah [majina ya madhehebu tofauti na ya maajabu]. Hakuna shaka yoyote kwamba hao ni makafiri.”

 

As-Swaarim al-Masluul, 3/1108-1110.

 

 

Ibn Hazm amesema:

 

“Maoni kwamba Qur-aan imegeuzwa ni ukafiri wa waziwazi na kukana yale ambayo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema.”

 

Al-Faswl fi’l-Ahwaa wal-Milal wan-Nihal, 4/139.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Surah hiyo inaweza kupatikana pia katika kiungo kifuatacho:

 

http://www.islamicweb.com/?folder=beliefs

 

 

 *Picha na Surah hiyo wanayodai Mashia kuwa imeshushwa kwa ajili ya 'Aliy bin Abi Twaalib.

     سورة الولاية  هذه صور فوتوغرافية يعتقد الشيعة هداهم الله انها كانت في القرأن اكريم

 

 

 ولا نقول إلا لَعْنةَ اللَّهِ عَلَى الْكَاذِبِينَ

 

سورة الولاية وسورة النورين اللتان يدعي علماء الشيعه أنهما حذفتا من القرآن الكريم .

 

1 -   سورة النورين { يا أيها الذين آمنوا آمنوا بالنورين أنزلناهما يتلوان عليكم آياتي ويحذرانكم عذاب يوم عظيم نوران بعضهما من بعض وأنا السميع العليم إن الذين يوفون ورسوله في آيات لهم جنات النعيم (كذا) والذين كفروا من بعد ما آمنوا بنقضهم ميثاقهم وما عاهدهم الرسول عليه يقذفون في الجحيم ظلموا أنفسهم وعصوا الوصي الرسول  أولئك يسقون من حميم إن الله الذي نور السموات والأرض بما شاء واصطفى من الملائكة وجعل من المؤمنين اولئك في خلقه يفعل الله ما يشاء لا إله إلا هو الرحمن الرحيم قد مكر الذين من قبلهم برسلهم فأخذهم بمكرهم إن أخذي شديد أليم إن الله قد أهلك عاداً وثمود بما كسبوا وجعلهم لكم تذكرة فلا تتفون وفرعون بما طغى على موسى وأخيه هارون أغرقته ومن تبعه أجمعين ليكون لكم آية وإن أكثركم فاسقون إن الله يجمعهم في يوم الحشر فلا يستطيعون الجواب حين يسألون إن الجحيم مأواهم وأن الله عليم حكيم يا أيها الرسول بلغ إنذاري فسوف يعلمون قد خسر الذين كانوا عن آياتي وحكمي معرضون مثل الذين يوفون بعهدك أني جزيتهم جنات النعيم إن الله لذو مغفرة وأجر عظيم وإن علياً من المتقين وإنا لنوفيه حقه يوم الدين ما نحن عن ظلمه بغافلين وكرمناه على أهلك أجمعين فإنه وذريته لصابرون وأن عدوهم إمام المجرمين قل للذين كفروا بعد ما آمنوا طلبتم زينة الحياة الدنيا واستعجلتم بها ونسيتم ما وعدكم الله ورسوله ونقضتم العهود من بعد توكيدها وقد ضربنا لكم الأمثال لعلكم تهتدون يا أيها الرسول قد أنزلنا إليك آيات بينات فيها من يتوفاه مؤمناً ومن يتوليه من بعدك يظهرون فأعرض عنهم إنهم معرضون إنا لهم محضرون في يوم لا يغني عنهم شيء ولا هم يرحمون إن لهم جهنم مقاماً عنه لا يعدلون فسبح باسم ربك وكن من الساجدين ولقد أرسلنا موسى وهارون بما استخلف فبغوا هارون فصبر جميل فجعلنا منهم القردة والخنازير ولعناهم الى يوم يبعثون فاصبر فسوف يبصرون ولقد آتينا لك الحكم كالذين من قبلك من المرسلين وجعلنا لك منهم وصياً لعلهم يرجعون .  ومن يتولى عن أمري فإني مرجعه فليتمتعوا بكفرهم قليلاً فلا تسأل عن الناكثين يا أيها الرسول قد جعلنا لك في أعناق الذين آمنوا عهداً فخذه وكن من الشاكرين إن علياً قانتاً  بالليل ساجداً يحذر الآخرة ويرجو ثواب ربه قل هل يستوي الذين ظلموا وهم بعذابي يعلمون سنجعل الأغلال في أعناقهم وهم على أعمالهم يندمون إنا بشرناك بذريته الصالحين وإنهم لأمرنا لا يخلفون فعليهم مني صلوات ورحمة أحياء وأموتاً يوم يبعثون وعلى الذين يبغون عليهم من بعدك غضبي إنهم قوم سوء خاسرين وعلى الذين سلكوا مسلكهم مني رحمة وهم في الغرفات آمنون والحمد لله رب العالمين.

 

2 -  { يا أيها الذين آمنوا آمنوا بالنبي والولي اللذين بعثناهما يهديانكم الى صراط مستقيم نبي وولي بعضهما من بعض ، وأنا العليم الخبير ، إن الذين يوفون بعهد الله لهم جنات النعيم ، فالذين إذا تليت عليهم آياتنا كانوا بآياتنا مكذبين ، إن لهم في جهنم مقام عظيم ، نودي لهم يوم القيامة أين الضالون المكذبون للمرسلين ،  ما خلفهم المرسلين إلا بالحق ، وما كان الله لنظر هم الى أجل قريب فسبح بحمد ربك وعلي من الشاهدين }.

-    ذكر هذه السورة :

 أ )  العلامة النوري الطبرسي في كتابه فصل الخطاب في اثبات تحريف كتاب رب الارباب ص 180 .

 ب)  العلامة محمد باقر المجلسي في كتابه تذكرة الائمة ص 18 ، 19  باللغة الفارسية  منشورات مولانا .

 جـ)  كتاب (دبستان مذاهب ) باللغة الفارسية .

 د )  العلامة المحقق ميرزا حبيب الله الهاشمي الخوئي في كتابه (منهاج البراعة في شرح نهج البلاغه )  جـ2 ص 217.

 

-    ذكر هذه السورة:

  أ )  العلامة المحقق ميرزا حبيب الله الهاشمي الخوئي في كتابه (منهاج البراعة في شرح نهج البلاغه )  جـ2 ص 217..

  ب)  العلامة محمد باقر المجلسي في كتابه تذكرة الائمة ص 19 ، 20  باللغة الفارسية  منشورات مولانا  ، ايران .

 

 

Share