Transplant Na Kusaini Fomu Ya Kutumika Viungo Baada Ya Kufa

SWALI LA KWANZA:

Je Uislamu umeihalalisha transplant?

 

SWALI LA PILI:

Je inafaa muislamu kutiwa kiungo/organ cha aliyekuwa si muislamu?


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu Muislamu kutiwa viungo vya mtu mwengine.

Uislamu unatazama maslahi ya mwanaadamu na afya yake kwa ujumla. Ikiwa matibabu yako yatakuwa katika kutiwa kiungo basi Uislamu umekubaliana na mpango huo bila ya wasiwasi. Na haidhuru viungo hivi ambavyo anatiwa ni vya kutoka kwa Muislamu au asiyekuwa Muislamu. Bora tu kiungo anachotiwa kiwe ni kizuri sio kibovu na hakitomletea madhara kwa ubovu wake ikiwa kilikuwa hivyo.

 

Na kuna swahaba aliyekatwa pua katika Jihaad na akawa ni mwenye kutiwa pua iliyotengenezwa na dhahabu wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share