Kurudi Kwa Nabiy ‘Iysaa (عَلَيْهِ السَّلام) Na Kumua Masiyhud-Dajjaal Ni Kweli?

SWALI:

Asalam Aleikum WarahmatuLlahi wabarakatu, Naomba nifahamishwe vizuri kuhusu kureje kwa Nabii Issa (Aleihi Salaam). Kuna mambo ambayo yanayotatiza kuhusu kurejea kwake. Kwanza Nabii Issa alitumwa na Allaah kwa Umma wa Banii Israil ambao walimkataa na kukufuru na alikuja na injili ambayo wakristo wametengeneza yao. Jambo linalonitatiza ni kuwa sisi ni umma wa Mohammad (S.A.W) NA TUMEFUNDISHWA KUWA HAKUNA MTUME MWINGINE ATAKAE KUJA BAADA YAKE NA KITABU CHA KORAN NI MWISHO (LAST TESTAMENT). NA WAKRISTO WANADAI NABII ISSA (YESU) ATAKUJA KU-UOKOA ULIMWENGU NA KUMUUA ANAEMPINGA YEYE (ANT-CHRIST) NA SISI WAISLAMU TUNASEMA ATAKUJA KUVUNJA MISALABA NA KUMUUA MASIHI DAJJAL (ANTI CHRIST) NA NI KWELI IMANI YETU HAITIMII MPAKA TUAMINI NABII ISSA KURUDI?


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kurudi kwa Nabii ‘Iysa (‘alayhis Salaam).

Sisi Waislamu hatuna shida, tatizo wala utata kuhusiana na Nabii ‘Iysa (‘alayhis Salaam) kwani Allaah Aliyetukuka na Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wametuelezea kila kitu kuhusu yeye, kuanzia kuzaliwa kwake, utoto wake, kupazwa kwake mbinguni pasi na kuuliwa na Mayahudi na pia kurudi kwake.

Mayahudi na Wakristo wana yao kuhusiana na Masihi mtarajiwa kwa miono yao au maandiko yao. Nasi kama Waislamu tunao yetu ambayo mengine yanafanana na yao na mengine ni yetu khaswa yasiyofanana kabisa na waliyonao wao. Hadiyth sahihi za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) zimetuelezea kwa kina kuhusu kurudi tena Nabii ‘Iysa (‘Alayhis Salaam). Kuja kwake si kuendelesha utume wake bali ni kufuata yale yote aliyokuja nayo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa njia ambayo atakapokuja hatokuwa ni mwenye kuswalisha bali atamuacha Imaam wa Waislamu awe ni mwenye kuongoza Swalaah.

Hili ni suala muhimu la kiimani na jambo la kuamini ghaibu. Na kuamini mambo ya ghaibu ni katika mambo ya Ki-Itikadi na Imani. Allaah Aliyetukuka Amewasifu wale wenye kuamini ya ghaibu kwa kusema:

Ambao huyaamini ya ghaibu na husimamisha Swalah, na hutoa katika tuliyowapa. Na ambao wanayaamini yaliyoteremshwa kwako, na yaliyoteremshwa kabla yako; na Akhera wana yakini nayo” (al-Baqarah [2]: 3 – 4).

Bonyeza upate manufaa  zaidi:

Hadiyth Ya Al-Jassaasah

Nabii ‘Iysa Atakua Katika Kundi Gani Miongoni Mwa Makundi 72?

Nabii ‘Iysa Ametabiriwa Katika Qur-aan Kuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)?

Nani Aliyesulubiwa Badala ya Nabii 'Iysa ('Alayhis Salaam)?

Nini Ukweli Kuhusu Kupandishwa Nabii 'Iysa عليه السلام

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share