Anaswali Na Kusoma Qur-aan Lakini Anapenda Kufanya Maasi

 

Anaswali Na Kusoma Qur-aan Lakini Anapenda Kufanya Maasi

 

Alhidaaya.com

 

Swali:

 

Mimi ni mume wa kiislam na naomba mnisaidie nahitaji msaada. mimi usali usoma Quran na madua kwa wengi shida yangu kisha na penda kufanya maasi naomba msaada ya kuacha ya mambo shukuran.

 

A/alikum mimi ni kijana wakiume na penda kusali, kusoma quran na dua kwa wingi ila yangu na penda kuangali machafu kila sampuli, naomba mnisaidie niwe katika mja mwema. shukuran

 

Jibu:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho. 

 

Hili ni tatizo ambalo wengi miongoni mwetu Waislamu huwa tunakumbana nalo. Na sababu kubwa kutokea hayo huenda ni:

 

1.   Kuswali na kusoma Qur-aan kiada, yaani niliwakuta wazazi wakifanya hayo nami nafanya hayo bila ujuzi wa aina yoyote.

  

2.   Kutojua maana ya maneno ya Qur-aan mtu anayoyasoma hivyo huenda ikawa Qur-aan inamlaani mmoja wetu naye anaona yupo mahali pazuri.

 

3.     Kutokuwa na Ikhlaasw katika kutokeleza ‘Ibaadah hizi mbili na nyenginezo.

 

4.     Ukosefu wa elimu kuhusiana na halali na haramu katika Uislamu.

  

5.     Marafiki wabaya wenye kumshawishi mmoja wetu kufanya hayo.

 

Ikiwa tatizo hilo ambalo linamkumba mmoja wetu ni lazima mkosa ajitahidi sana kurekebisha hali hiyo bila kuchelewa. La sivyo, atajikuta pabaya sana. Kwa hivyo, linalotakiwa ni mtu kusoma Qur-aan pamoja na kujua maana yake. Jambo hilo ndilo lililowabadilisha Waarabu wakati wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) waliokuwa katika kiza totoro kubadilika na kuwa ni mwangaza kwa ulimwengu mzima. Si kusoma tu na kujua maana bali kufanya bidii na juhudi kutekeleza yaliyo ndani yake.

 

Mtu akifanya juhudi hiyo basi Allaah Aliyetukuka naye Humtilia tawfiki katika kuyaendea mema na mazuri. Kuwa na marafiki wema na wazuri ambao mtasaidiana katika kuyaendea mema na kuacha mabaya.

 

Na kumbuka maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anayosema:

إِنَّ الصَّلَاةَ تَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ ۗ

Hakika Swalaah inazuia machafu na munkari. [Al-‘Ankabuut: 45]

 

Na In shaa Allaah hali hiyo itabadilika na wala usikate tamaa kwani Allaah Aliyetukuka Humbadilisha mwenye Niyah ya kubadilika. Na bila shaka wewe na wengine tutakuwa miongoni mwa hao wenye kubadilika na kuwa karibu sana na Muumba wetu.

 

Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:

 

Anapenda Kuangalia Machafu Kisha Anatubu, Kisha Anarudia Tena, Naye Anachukiwa Jambo Hili

 

Anajaribu Kufanya Mema Lakini Ana Tabia Chafu Ya Kuondosha Matamanio Kwa Mkono Na Vifaa, Afanyeje Kujiepusha Shaytwaan ?

 

Anaomba Toba Kisha Anarudia Tena Kufanya Kosa Kila Mara. Vipi Aweze Kuimarika Bila Kurudi Makosani?

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share