Amedai Talaka, Anasema Sababu Ni Husda Na Shaytwaan

SWALI:

 

Assalamu Allaykum Warahmatullahi Wabarakatuh.

 

Nimeowana na mke wangu kwa muda wa miaka kumi, na tuna watoto wawili wadogo. Ghafla mwaka jana alianza kunidai talaka bila ya sababu ya msingi tumekwisha kila njia kutafuta sababu lakini tumeshindwa, kitu kikubwa alosema kuwa yeye amenichukia mie mumewe bila ya sababu hajui kafikwa na nini anaamin ni HUSDA au SHETANI. Aliondoka hapa ulaya na kwenda zake kwao Zanzibar na kuzidi kudai talaka kila nikiongea nae kwenye simu. Suala langu talaka niliomtamkia kwenye simu inahisabika kuwa talaka? Na haya mambo ya HUSDA na SHETANI ni kweli yapo au ananizuzua tu?

 

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu mke anayedai talaka na wewe ukamtamkiya kwenye simu.

Ama kuhusu mas-ala ya talaka, hili ni jambop ambalo halina mzaha katika Uislamu. Kwa hiyo, ukitamka tu hata kwa njia ya simu au kwa njia yoyote inayoeleweka na iliyo wazi basi talaka inakuwa imepita. Kwa hiyo, ikiwa umemtamkia kwenye simu talaka hiyo itakuwa imepita.

 

Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:

 

 

Talaka Inayotolewa Kwa Njia Ya Simu Inapita?

 

Mume Kamtamkia Mkewe Talaka Kisha Akataka Kumrejea Katika Eda, Mwanamke Anayo Haki Kukataa Kurudiana Na Mumewe?

 

Mas-ala Ya Talaka Mbali Mbali

 

Ameandika Talaka Miezi Minne Nyuma Ila Alikuwa Anasita, Mwishowe Amemtamkia Mkewe Talaka, Mke Ahesabu Ametalikiwa Tokea Lini?

 

Talaka Ziko Aina Ngapi Na Wakati Gani Zinasihi?

 

 

Hata hivyo unaweza kumrudia bila ndoa mpya kabla ya eda yake kumalizika. Ama eda ikimalizika itabidi umpose, utoe mahari na umuoe tena upya.

 

Ama suala kuhusu husda na Mashaytwaan ipo na wapo. Na mtu huweza kuathirika kwa ajili ya husda au Mashaytwaan ambao wanadhuru wanaadamu. Kwa hiyo, linahitajika si kumpeleka mtalaka wako kwa wachawi au wapigaji bao lakini umpeleke kwa Shaykh, mcha Mungu na mzoefu katika usomeaji wa Ruqyah na InshaAllaah hayo anayohisi yatapotea kabisa.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share