Samaki Wa Tuna Katika Mzungurisho Wa Mkate Wa Pita-Pan

Samaki Wa Tuna Katika Mzungurisho Wa Mkate Wa Pita-Pan

Vipimo

Vipande vya Samaki wa Tuna (flaked) - 3 Vikopo

Karoti - 2

Kabeji (Cabbage) - ¼

Pilipili boga jekundu (capsicum) - 1

Parsley (aina ya kotmiri) - 3 msongo (bunch)

Pilipili manga - 1 kijiko cha chai

Ndimu - 2

Jibini yam alai (Cream cheese) - 4 vijiko vya supu

Mikate ya Pita - 2 mikubwa

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 1. Menya karoti kisha kuna (grate) weka kando.
 2. Katakata kabeji nyembaba weka kando.
 3. Katakata pilipili boga (capsicum) ndogo weka kando.
 4. Katakata parsley ndogo ndogo (chopped) weka kando.
 5. Weka samaki katika chombo cha kukaangia (frying pan) au karai kisha kamulia  ndimu, tia chumvi na pilipili manga.
 6. Kausha katika moto mdogo kiasi tu cha kuchanganyika na samaki wa tuna kupashika moto vizuri.
 7. Epua weka katika bakuli kubwa.
 8. Tia karoti, kabeji, pilipili boga, parsley changanya vizuri.
 9. Pakaza jibini ya malai (cream cheese) katika mkate wa Pita (Pita  bread).
 10. Weka mchanganyiko kama ilivyo katika picha.
 11. Zunguruisha hadi mwisho wa mkate kisha katakata vipande panga katika sahani ya kupakulia ikiwa tayari.

             

 

 

 

 

Share