Ana Haki Kudai Talaka Ikiwa Mume Hawezi Tendo La Ndoa?

SWALI:

 

asalaam alaykum warahmatullahi wabarakat, naam sheikh mm nimfatiliaji mzuri wamakala zenu. na inshaallah Mwenyezi Mungu awape hidaya kwa kutuelimisha tusioyajua. mimi swali langu nnamume ambae anamatatizo ya nguvu za kume. Tushahangaika sana hospital, ktk dawa za kisunnah bado haijakuwa soud. na mimi bado msichana mdogo jee nnahaki yakudai talaka?

nimulizia kwa mashekhe huku tz wamesema mpaka iwe sijafanya tendo la ndoa kwa mwaka mzima. na sisi huwatunakaa miezi kimi ndo anaweza siku moja, tunakaa tena miezi kumi na moja. jee hapo ni swahihi namimi binaadam nnamatamanio. nasiwezikuzini. naomba jibu tafadhali, WABILLAHI TAUFIK WA SALAAM ALAYKUM WARAHMATULLAHI WABARAKAAT


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu mumeo kutoweza kufanya tendo la ndoa.

Msingi wa Dini hii ni kutodhulumu wala kutodhulumiwa. Ndio Mtume wetu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akatuambia:

Haifai kudhuru wala kulipana madhara” (Ibn Maajah, Maalik na ad-Daaraqutwniy).

 

Mume kutojiweza ni sababu moja ya mke kuomba talaka na ni haki kwake kupewa na Qaadhi ikiwa mume amekataa kuitoa.

 

Miezi kumi au kumi na moja ni mingi kwa mwanamke kuweza kuvumilia na kuvumilia huko kunamfanya awe ni mwenye kudhulumika. Ni kwa ajili ya hiyo ndio ‘Umar bin al-Khatwtwaab (Radhiya Allaahu ‘anhu) akaaamrisha kuwa haifai kwa waume walio kwenye Jihaad kukaa zaidi ya miezi minne bila kuja kuwatazama na kukaa kwa muda na wake zao.

 Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:

 

Anafaa Kuachika Ikiwa Mume Hawezi Tendo La Ndoa?

Mume Hamtoshelezei Matamanio Yake Ya Tendo La Ndoa, Anaomba Ushauri

Mume Kahama Chumba Kwa Miezi 3 Hafanyi Tendo La Ndoa, Akiulizwa Anasema Anachoka Kazini

Mke Analalamika Mume Ana Mashetani Yanamfanya Asiweze Kukamilisha Tendo La Ndoa

Anampenda Sana Mume Wake Lakini Hawana Raha Katika Tendo La Ndoa, Wafanyeje?

Mume Au Mke Hawezi Tendo La Ndoa Kwa Zaidi Ya Miaka 5, Hukmu Ni Nini?

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share