Wasiwasi Wa Qiblah Kilipo

SWALI:

 

Natumai ya kua ni wazima wa Afya na M/Mungu awazidishie Imman zaidi na zaidi katika kutuelewesha yaliyomo kwenye dinii hii tukuf Kiufupi nimekua gizani kwa muda mrefu katika mambo ya dini. Namshukur M/Mungu tokea niigundue tovuti hii imeniweka kifua mbele kayika kuyafuatilia mambo ya dini yangu Samahanini sana Nilikua Nna swali langu nataka kuliuliza Ijapo kua hapa sio sehem yake!!

 

Mimi kwa sasa ninaish kwnye nchi za magharib {ulaya} na sehem ninapoish hapana Mskiti!! Kiufupi naswali ndani kwangu Lakini mara nyingi huwa napatwa na wasiwasi na sehem ya kibla Je nifanye nini ili niondowe wasi wasi huu na nikipate kibla?


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu wasiwasi wa kukipata Qiblah.

 

Huhitaji kuwa na wasiwasi kuhusiana na Qiblah. Jambo ambalo unafaa ufanye ni kujitahidi kutafuta Qiblah kwa kujua jeografia japokuwa kidogo. Kuwa na ramani itakayo kuongoza kujua wewe upo wapi na Makkah ipo sehemu gani. Je, Makkah ipo kusini ya sehemu uliyopo au mashariki. Ukisha kujua hilo itakuwa ni rahisi sana kuelekea Qiblah.

 

Na rahisi zaidi ni kununua mswala ambao una compass. Kwa kufanya hivyo utakuwa popote duniani utakapokuwa utaweza kuelekea Qiblah bila ya shida au wasiwasi wowote.

 

Njia nyingine hata kama hakuna Msikiti hapo karibu, ni kutafuta Muislam hapo ulipo na umuulize akujulishe Qiblah kilipo kwa hilo eneo lako wewe.

 

Na hata ikitokea kuwa baada ya kujitahidi kujua Qiblah kwa kuwa huna mswala wa compass na badaye ukagundua kuwa umekosea Swalaah yako bado ni sawa mbele ya Allaah Aliyetukuka.

 

Tafadhali bonyeza kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:

 

Vipi Kutambua Qiblah Ikiwa Hujui Kiko Wapi

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share