Mashia Na Njama Za Kupenyeza Itikadi Zao Za Kikafiri Kwenye Sinema Za ‘Dini’

 

 

Mashia Na Njama Za Kupenyeza Itikadi Zao Za Kikafiri Kwenye Sinema Za ‘Dini’

 

Alhidaaya.com

 

Kuna mbinu na hila nyingi zinafanyika katika kuuvuruga Uislamu na hata kuungamiza. Mbinu na hila hizo zinafanywa na maadui wa nje na maadui wa ndani wa dini hii.

 

 

Maadui wa nje wote tunawajua. Lakini maadui wa ndani ni wachache wanaowajua na wengi huwaona ni wenzetu na wengi wanawaona ndio labda watetezi wa Uislamu na hasa hasa baada ya nchi za Kiarabu kuonekana legelege na wanashirikiana na makafiri katika mambo yao. Wengi wakadanganyika na misimamo ya juu juu ya Iran na wafursi na wakaona kwa misimamo yao ya kisiasa na kuwa kijuu juu wanaonekana wana uadui na nchi za Magharibi na kuwa na kauli za kutishatisha, hilo likawadanganya sana hasa wanaojiona ni wasomi wa kisekula na kuona Iran au Mashia ndio wanaowakilisha Uislamu!

 

 

Matokeo yake, watu wakawa wanakumbwa na wimbi hilo la misimamo ya kisiasa na kutumbukia katika upotofu wa kiitikadi na kuishia kuwa Mashia. Inna LiLLaahi wa inna ilayhi raji'uun.

 

 

Ni rahisi sana kuweza kujiepusha na uadui wa hawa Makafiri na Mayahudi, kwani wao wanakuonesha wazi wazi kama hawakupendi. Njama na propaganda za Mashia dhidi ya Waislamu ni vigumu sana kuweza kuzigundua kwani wao wamevaa na kudhihirisha vazi la Kiislamu, ila kinachochezwa ndani ya pazia ni Ukafiri na njama za kutaka kupotosha watu na itikadi zao potevu. Ndiyo maana wakati mwingine ni vigumu kuelewa na bado utasikia baadhi ya watu wanalilia umoja na kila atamkaye shahada tu.

 

 

Wao kwa akili zao wanafikiria kwamba kuwa wengi na kila mmoja na taka zake ndiyo utatufanya kupata Nusra ya Allah (Subhaanahu wa Ta'ala). Nusra haipatikani mpaka watu walinganie kwenye tawhiyd na wawe na 'Aqiydah sahihi iliyofungamana chini ya kitabu cha Allaah na Sunnah sahihi kwa ufahamu wa wema waliyotangulia.

 

 

Inakadiriwa kwamba Mashia wote ulimwenguni wanaweza kuwa asilimia 10 mpaka 15%. Ambapo wengi wao wanaishi Iran na Iraq. Na huko ndiko kwenye asili haswa ya uchafu wa Mashia na Ushia. Iran ndiyo nchi ya kwanza katika mji mkuu wake, Tehran isiyokuwa na msitiki wa Kisunni ilihali wamajusi (Wanaoabudu Moto), Mayahudi na Manaswara na hata Hindu wana mahekalu yao.

 

 

Tehran, mji mkuu wa Iran, kuna jengo kubwa liko tena chini ya serikali ambalo lina kaburi la yule muuaji aliyemuua Khalifa wa pili wa Uislamu, ‘Umar bin Khattaab (Radhiya Allaahu ‘anhu) na Mashia wakilizuru kaburi la muuaji huyo na kusherehekea na kumuombea na kumsifu kwa kumuua Khalifa mtukufu muongofu wa Uislamu!! Pamoja na nchi za kisuni nyingi kulalamikia hilo, lakini mpaka leo serikali ya Iran imekaa kimya na kuacha hali hiyo ya uadui na chuki iendelee.

 

 

Nchi ambayo ukimwita mtoto wako jina la vipenzi vya Allaah na Mtume wake kama Abu Bakr, 'Umar, 'Uthmaan, 'Aaishah (Radhi za Allah ziwashukiye wote) na n.k basi ni jarima na utajiweka kwenye matatizo makubwa.

 

Utaruhusiwa kuwapatia watoto wako moja ya majina hayo, ikiwa tu utakubaliana na fikra yao chafu ya kumpiga mtoto kila mara unapojihisi dhiki au hasira. Basi unampiga huku ukitoa matusi na kuchukulia kama kweli ni Abu Bakr au 'Umar. Hiyo ndiyo hali halisi ilipofikia!!

 

 

Kutokana na uchache wao, wanajaribu kila siku kupenyeza huku na kule nchi tofauti katika nyanja za juu kama za Makamu wa raisi, Waziri, Vyuo vya kiislamu na n.k ilimradi tu waweze kufikia malengo yao ya kupenyeza itikadi yao mbovu na chafu. Na mpaka hivi leo wanatumia nafasi kubwa sana katika jamii ili tu wafikie lengo lao hilo la mda mrefu. Baada ya kuona kwamba si rahisi na baadhi ya Masunni wapo macho na wapo imara, sasa hivi leo wameamua kutumia njia mbali mbali za kueneza itikadi na mafunzo mabovu kwenye jamii ya Kiislamu. Tumeshawagundua mahali tofauti na kwenye tovuti mbali mbali huku wakiwa makini sana kutojulikana ni watu gani na wanafikra gani.

 

 

Na mara nyingi inakuwa ni vigumu sana kuwagundua ila baada ya kipindi kirefu; kwani mfano wao ni kama Simba apanuwapo kinywa ukadhani anacheka kumbe analenga jambo fulani. Sasa imekuwa ni kila upenyo wanaoupata wanaingiza itikadi yao chafu na mbovu.

 

 

Mashia wametengeneza filamu kumhusu Nabii Yuusuf ('Alayhis Salaam) na filamu hiyo kwa aina ya 'series' (Musalsal) ina karibu vipande (Parts) 45 kimeonyeshwa kwenye nchi kadhaa za Kiarabu na imetengenzwa na Mashia wa Lebanon na wachezaji wa sinema wa Iran.

 

Kimepata umaarufu sana, lakini wamemuonyesha Nabii wa Allaah kwa sura na kumweka mtu kumuiga kama kwamba huyo mtu ana sifa safi na tukufu kama za Nabii!! Na hali mtu huyo ni mchezaji sinema na ni mchafu tu kama wacheza sinema wengi!

 

Mashia wamekitumia kisa hicho na kupata umaarufu sana kwenye nchi za Kiarabu hata watu wanapoambiwa haifai kutazama filamu kama hizo hawasikii na hawaelewi, kinyume chake wanasifia sana na kushinda kutwa nzima wakiangalia!

 

Kadhalika wamemmathil Jibriyl ('Alayhis Salaam) kama mtu anayekuja kumpa wahyi Yuusuf na baba yake!

 

 

Kwa mukhtasari, wameonesha Malaika Jibriyl ('Alayhis Salaam) amekuja kwa umbo la kuigiza mpaka kwa Nabii Yuusuf ('Alayhis Salaam). Baya zaidi ni kwamba wanajaribu kupenyeza itikadi zao potevu ndani ya filamu hizo, eti Jibriyl akamwendea Nabii Yuusuf alipokuwa kwenye kishimo na kumwambia “Omba kwa jina la Mtume na Maimamu 12”!! Yaani Nabii Yuusuf afanye Tawassul akiwa kisimani kwa maimamu 12 wa Kishia ili aokoke!? Tazameni hatari ya hiyo itikadi na hatari ya hawa watu kupenyeza Ushia wao mpaka kwenye sinema za dini. Hata hizo sinema wanaziingiza Ushia!! Kisha wapi na wapi Nabii Yuusuf na maimamu 12 wa kishia??

 

Mashia kwao hakuna tatizo kumtengeneza au kumchora Mtume/Mitume au Maimamu wao 12!!!

 

Kwa wale mashia wenye itikadi kali haswa wa huko Iran na Iraq, asilimia kubwa wanakuwa na mapicha ya hao maimamu wao kwenye mahekalu yao mpaka kwenye majumba yao.

 

 

Mashia wametumia ujanja huo na kutengeneza filamu nyingi za kuhusu Mitume na kuhusu Historia ya Kiislamu!! Hata ile filamu inayoitwa 'Ar-Rissaalah' (The Message) ambayo imeenea na kupata umaarufu dunia nzima, wao wana mkono ndani yake kama kumzulia Hind kula ini la Hamzah (Radhiya Allaahu 'anhu) baada ya kuuliwa n.k. Na fikira hiyo imepandikizwa hata kwa masuni wengi na wameiamini na wakiisadia kuitangaza!

 

Na wametengeneza filamu za Nabii 'Iysaa na Maryam ('Aalayhimas Salaam) na zingine nyingi na hivyo kuingiza fikra zao za Kishia potevu na watu wengi hawajagundua. Na zimetazamwa sana na watu wengi na ingawa zimetengenezwa kwa lugha ya Kifursi (Iran) na zingine kwa Kiarabu, lakini zimefasiriwa kwa lugha nyingi sana.

 

 

Jambo la kusikitisha sana, ni kwamba filamu hizo zinauzwa sasa kwenye maduka ya Mashia na maduka hata ya Masuni mbele ya Msikiti wa Mtoro Dar es Salaam, na duka la Msikiti wa Maibadhi ambapo kuna ndugu mmoja alipata kopi zake huko katika duka la 'Istiqaamah' la Maibaadhi la mtaa wa Ilala, Dar es Salaam ambapo inaonekana imerekodiwa kutoka kwenye TV ya hao Mashia! Isitoshe siku hizi sinema hizo zinafanyiwa tarjama za kiswahili na watu wengi wanavutika nazo kwa kuwa wanaziona kwa lugha wanayoifahamu na hivyo hatari kuzidi kuwa kubwa zaidi na zaidi.

 

 

Tunachukua fursa hii kuwatanabahisha/kuwanasihi ndugu zetu waislamu ulimwenguni, kwanza kujiweka mbali na kununua au kuuza au kuzifasiri sinema kama hizi, vilevile kutoangamiza mda wao kwa kuangalia filamu hizi za uongo na zenye fikra chafu. Kwa maana kuna hatari za watu wa kawaida wasio na elimu kuathirika na kuchukua historia ya uongo isiyo sahihi yenye mielekeo ya Kishia na mielekeo ya kishirikina ndani yake.

 

 

Vilevile tusambaze ujumbe huu kwa waislamu wengine ili wasije kuangamiza pesa zao kwa kuzinunua na kushinda kwa kuziangalia. Na kwa yeyote utayemuona anashiriki katika kuzinunua, kuzisambaza au hata kuangalia basi tuwe wepesi kunasihiana na kukumbushana.

 

 

Muislamu hapaswi kupoteza mda wake katika kuangalia mambo ya kipuuzi yasiyokuwa na faida na Akhera yako wala Dunia yako. Kumbuka kuwa mda ndiyo umri wako wote, na kila dakika inapokwenda basi jua kuwa inakusogeza kwenye kaburi lako. Na kila dakika utaulizwa uliitumia kwenye kufanya nini!

 

 

Kwahiyo ni masikitiko muislamu kushinda kwenye TV na kuangalia filamu mbovu za Mashia akiitakidi yuko katika kheri. Waislamu wengine kushinda kwenye TV na kuangalia Filamu za kizungu, maigizo ya ki-Tanzania, ki-Kenya, ki-Nigeria, musalsal (Series), na michezo mbali mbali isiyokuwa na faida yoyote bali madhara ndiyo mengi sana kuliko hata faida. Na hii ni hasara na madhara makubwa sana yaliyoenea kwenye jamii yetu ya Kiislamu na kupoteza muda na hata kuharibu maadili. Ukiongezea na mabalaa ya muziki ya bongo fleva na miziki mingine michafu!

 

 

Tunamuomba Allaah Muweza wa kila jambo Atuepushe na shari ya hawa Mashia. Atuweke mbali na mafunzo machafu wanayojaribu kupenyezwa na maadui wa dini hii. Ailinde dini Yake na wale wote wanaolinda mafunzo Yake sahihi aliyokuja nayo Mtume wetu Muhammad (Swala Allahu 'alayhi wa sallam).

 

 

Je, vipi inaingiaje akilini kwa hawa Mashia hata mtu ufikie kuthubutu kuwamathili Mitume wa Allaah ('Alayhimus Salaam) na Swahaba zake (Radhi za Allaah Ziwashukiye wote)? Ni yupi ajuwae kama wanafanana hivyo?? Hii ndio ile mila ya Manaswara ya kumfananisha Yesu na kumchora na kila mahali kuuzwa na kuenea hizo picha za Yesu.

 

 

Hao wacheza sinema ni watu wenye maadili yasiofaa kabisa na tena kumchukua mcheza sinema anaecheza sinema za mapenzi na uchafu kisha ukampa nafasi ya kumwiga mtu mwema tena kiumbe mtukufu, Nabii wa Allaah? Hilo pekee ni tusi kubwa kwa Nabii wa Allaah, wachilia mbali ushirikina na upotevu uliojaa ndani ya hizo sinema na udanganyifu wa historia sahihi ya Mitume na Uislamu kwa ujumla wake. 

 

 

Share