Mashairi: Allaah Wanusuru Ndugu Zetu Wa Dammaaj Na Uovu Wa Mashia

                     Abdallah Bin Eifan

                 (Jeddah, Saudi Arabia)

Salaam zangu natuma, zifike kwa Waumini,

Roho yangu inauma, na dukuduku moyoni,

Nina mengi ya kusema, naomba nisikilizeni,

Mola Wetu Wanusuru, ndugu zetu wa Dammaaj.

Naomba sikilizeni, na masikio tegeni,

Dammaaj kule Yemeni, ndugu wapo hatarini,

Wanauawa yakini, na Mashia makhaini,

Mola Wetu Wanusuru, ndugu zetu wa Dammaaj.

Huthi hao makatili, ni ndugu wa Mashetani,

Mambo yao ni batili, na tena hawana dini,

Husaidiwa kwa mali, na adui mu-Irani,

Mola Wetu Wanusuru, ndugu zetu wa Dammaaj.

Wazee na kina mama, na watoto wa shuleni,

Huchinjwa kama wanyama, kama vile machinjoni,

Wamekua mayatima, na mengi hatuyaoni,

Mola Wetu Wanusuru, ndugu zetu wa Dammaaj.

Chakula hata madawa, wananyimwa tazameni,

Hakuna wanachopewa, ila risasi mwilini,

Lini wataokolewa, ndugu zetu masikini,

Mola Wetu Wanusuru, ndugu zetu wa Dammaaj.

Hushindwa hata kutoka, wamefungiwa mjini,

Na mimba huharibika, wanakufa wanandani,

Wamebanwa kwa hakika, wamo kwenye mitihani,

Mola Wetu Wanusuru, ndugu zetu wa Dammaaj.

Ndugu wanahangaika, hakuna tena amani,

Wakati umeshafika, wa jihadi ikhwani,

Tena tufanye haraka, misaada tupelekeni,

Mola Wetu Wanusuru, ndugu zetu wa Dammaaj.

Vita vya Badri zamani, Mola wetu Rahmani,

Malaika toka mbinguni, Uliteremsha vitani, (Qur-aan: 8: 9 & 12)

Na mapanga mikononi, waliwapiga shingoni,

Mola Wetu Wanusuru, ndugu zetu wa Dammaaj.

Na Madina kumbukeni, walipigwa uwanjani,

Majeshi toka mbinguni, na kwa macho huwaoni, (Qur-aan: 33: 9)

Walishinda Waumini, kwa Msaada wa Manani,

Mola Wetu Wanusuru, ndugu zetu wa Dammaaj.

Waonyeshe Maulana, Nguvu Zako kwa makini,

Fimbo Yako kali sana, anaebisha ni nani ?

Kwa marefu na mapana, waangamize nchini,

Mola Wetu Wanusuru, ndugu zetu wa Dammaaj.

Tunakuomba Jalali, Wanusuru Waumini,

Ngumu sana yao hali, na sote tuna huzuni,

Watandike majahili, Mahuthi na tuwalaani,

Mola Wetu Wanusuru, ndugu zetu wa Dammaaj.

         Mahuthi ni wanafiki, Makafiri Mapagani,

         Mungu Uwatie dhiki, akhera na duniani,

         Hawaachi yao chuki, nyoyo hazina imani,

         Mola Wetu Wanusuru, ndugu zetu wa Dammaaj.

Ewe Mola Mtukufu, tupo tunatumaini,

Viumbe Vyako dhaifu, tunakuomba Manani,

Tunakuomba Raufu, Ututoe mashakani,

Mola Wetu Wanusuru, ndugu zetu wa Dammaaj.

Nafunga langu shairi, na machozi kifuani,

Tunafuatia habari, za ndugu kule Yemeni,

Tupate habari nzuri, Tufurahi tushukuru,

Mola Wetu Wanusuru, ndugu zetu wa Dammaaj.

Share