Maulidi: Vizuizi 12 Dhidi Ya Kusherehekea Kuzaliwa Kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Vizuizi 12 Dhidi Ya Kusherehekea Kuzaliwa Kwa

 

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)

 

Imetafsiriwa na Naaswir Haamid

 

Alhidaaya.com

 

 

Shukrani ni za Allaah, na rahma zimuendee Rasuli wake Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye ni mbora wa viumbe wote …

 

Ninataka kuweka (wazi) mbele ya msomaji, vizuizi (nukta) vifuatavyo kuhusiana na washerehekeaji wa siku ya kuzaliwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aailihi wa sallam), ikitajwa tendo lao la kufanya hivyo, kwa mujibu wa Shari’ah ya Kiislamu; kitendo cha haki iliyoruhusiwa (Halali) au dhidi ya Shari’ah (Haramu). Kwa maneno mengine, je inastahiki kupatiwa adhabu? Zaidi ninamuomba Allaah, kwamba makala hii kuwa ni yenye manufaa kwa wote.

 

Kizuizi Cha Kwanza

Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Amemtaka Nabiy  (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kufuata yale ambayo Allaah Amemshushia na sio kubuni maelekezo ya ‘uongo’, Anasema katika maneno Yake ndani ya Qur-aan:

 ثُمَّ جَعَلْنَاكَ عَلَىٰ شَرِيعَةٍ مِّنَ الْأَمْرِ فَاتَّبِعْهَا وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ

Kisha Tukakuwekea (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) shariy’ah ya mambo, basi ifuate, na wala usifuate hawaa za wale wasiojua. [Al-Jaathiyah: 18].

 

Matendo ya ibada ya Kiislamu hayabadiliki, hayaathiriki na yenye kudumu kama vile yalivyoshushuwa kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Akili haiwezi kutumika kuingilia ibada hizo. Hivyo, Allaah Amemuelekeza Nabiy wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kufuata wahyi (tu) katika nafasi nyingi. Kwa mfano maneno haya ya Allaah:

وَإِذَا لَمْ تَأْتِهِم بِآيَةٍ قَالُوا لَوْلَا اجْتَبَيْتَهَا ۚ قُلْ إِنَّمَا أَتَّبِعُ مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ مِن رَّبِّي ۚ هَـٰذَا بَصَائِرُ مِن رَّبِّكُمْ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ

Na usipowaletea Aayah (muujiza, ishara) husema: Kwanini hukuibuni? Sema: Hakika hapana ila nafuata yale nilofunuliwa Wahy kutoka kwa Rabb wangu. Hii (Qur-aan) ni nuru za elimu na umaizi kutoka kwa Rabb wenu, na ni mwongozo na rahmah kwa watu wanaoamini. [Al-A’raaf: 203].

 

Zaidi, Wanachuoni sahihi wa Uislamu wameamua kwamba: ibada ni kwa mujibu tu wa kufuata Qur-aan na Sunnah, na sio kuzua.

 

 

Kizuizi Cha Pili

Hakika Allaah Amewashushia ihsani kubwa Waumini kwa kuwaletea Nabiy wake Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na sio sherehe ya siku yake ya kuzaliwa hata kidogo. Kwamba yale ambayo Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) amesema ndani ya Kitabu Chake “Qur-aan” (ndio ya kufuatwa). Aayah zinazozungumzia kiini hichi itakuwa ni:

لَقَدْ مَنَّ اللَّـهُ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ إِذْ بَعَثَ فِيهِمْ رَسُولًا مِّنْ أَنفُسِهِمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَإِن كَانُوا مِن قَبْلُ لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ

Kwa yakini Allaah Amewafanyia fadhila Waumini pale Alipomtuma kwao, Rasuli miongoni mwao, anawasomea Aayaat Zake na anawatakasa na anawafunza Kitabu na Hikmah (Sunnah); japokuwa walikuwa kabla katika upotofu bayana. [Al-‘Imraan: 164].

 

 

Kizuizi Cha Tatu

Kizazi cha mwanzo cha Waumini ambacho kilikuwa ni cha Swahaba wa Nabiy (ambao tumehimizwa kuwafuata na kuchukua ufahamu wao wa kipi kilichotolewa maana ndani ya Aayah za Qur-aan na Hadiyth kuwa ndio kigezo cha ufahamu wetu wa Uislamu) hawakupatapo kuongeza kitu chochote katika ibada zao za kawaida katika siku ya kuzaliwa kwa Nabiy. Iwapo wameongeza cha ziada, hakuna shaka yoyote kwamba kingetufikia sisi. Kwa sababu walikuwa ni wenye hamu na hima ya kuwa na elimu sahihi kabisa kwa ajili ya kufanya matendo ya ibada yenye kumridhisha Allaah na ndivyo ilivyokuwa kwa kizazi kilichofuata na kizazi kilichofuata baadaye.

 

Mwanachuoni mwenye elimu; Abu ‘Abdillaah Muhammad Al-Haffaar (wa madhehebu ya Maalik), amesema kwamba: “Je hutambui kwamba “Ijumaa” ndio siku bora kwa siku zote, na tendo la ibada lililokuwa bora kabisa katika siku ni kuifunga, lakini Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametuzuia kuifunga juu ya kwamba ina fadhila kubwa. Hii inamaanisha kwamba tunazuiwa kubuni tendo la ibada kwa mnasaba wa wakati au sehemu. Kwamba kizazi cha mwisho cha taifa hili halitoongoka zaidi kuliko kizazi cha mwanzo. Kwa uaminifu (ninasema) Kheri zote zipo katika kufuata ‘Salafus Swaalih’ kizazi cha mwanzo.” [Al-Mi’iyaar Al-Mu’rib 7/99].

 

 

Kizuizi Cha Nne

Angalia katika ufahamu adhimu wa Al-Faaruwq, ‘Umar bin Al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu)  pale alipoanzisha Kalenda la Waislamu kwa kuhama Nabiy kwenda Al-Madiynah, ambayo inasimama kama ni alama ya ushindi wa Uislamu dhidi ya ujahili kuliko kuanza tarehe ya Waislamu kwa siku ya kuzaliwa kwake au siku ya kifo chake. Je unaelewa kwanini? Ni kuipa nguvu asili na ukweli juu ya urembo wa ibada na desturi.

 

 

Kizuizi Cha Tano

Wa mwanzo kuzua uzushi huu ndani ya Uislamu lilikuwa ni Taifa la Faatwimiyy (Mashia) mjini Cairo katika karne ya nne ya Hijri. Walizua sherehe sita za siku ya kuzaliwa; kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ‘Aliy, Faatwimah, Al-Hasan na Al-Husayn, (Radhwiya Allaahu ‘anhum) na siku ya kuzaliwa mfalme wao pia. Sherehe hizi ziliendelea hadi pale zilipobatilishwa na Al-Afdhwal bin Amiyr Al-Jiyuwsh, kabla ya kurudishwa tena katika utawala wa Al-Haakim biamriLlaah katika mwaka 524 Milaadiy, kipindi ambacho watu walikuwa tayari washakaribia kuzisahau.

 

Haikuwahi kushuhudiwa sherehe hizi kabla ya taifa hilo. Suala ni kwamba: Je taifa hili lilikuwa na sifa za sisi kulifuata? (Taifa) ambalo linasimama dhidi ya misingi na nguzo za Uislamu?

 

Juu ya hayo, kitu kinachoshangaza ni kwamba baadhi ya watu wananasibisha siku ya kuzaliwa Mtume katika Laylatul-Qadr!

 

 

Kizuizi Cha Sita

Wanahistoria hawakuwa na makubaliano juu ya mwezi gani ambao Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amezaliwa. Baadhi wamesema ni Ramadhwaan, lakini Wanachuoni walio wengi wamesema kuwa ulikuwa ni mwezi wa Rabiy’ul Awwal. Halikadhalika, wamekhitalifiana pia katika siku yake ya kuzaliwa, kwa kauli zifuatazo:

 

Ibn ‘Abdil-Barr anasema ni siku ya pili ya Rabiy’ul Awwal. Ibn Hazm amesema ilikuwa ni siku ya nane ambayo ndio kauli waliyoichagua Wanachuoni wengi wa Hadiyth. Ingawa wengine wamesema kwamba ilikuwa ni siku ya tisa ambayo imekubaliwa kuwezekana kuzaliwa siku hiyo na Abu Al-Hasan na Zaahid Al-Kawthariy.

 

Ibn Is-haaq amesema kwamba ilikuwa ni siku ya kumi na mbili. Na kuna waliosema kuwa ni siku ya kumi na saba na kumi na nane ya mwezi huo.

 

Kutofautiana huku katika siku ya kuzaliwa Nabiy ni ushahidi wa kwamba Swahaba hawakuwa na hima ya kuifikisha kwa kizazi chengine siku hiyo, na kwamba kwa ufahamu wao haikuwemo ndani yake (siku hiyo ya kuzaliwa Nabiy) aina mahsusi ya ibada. Hivyo, iwapo kulikuwa na ibada maalumu ndani ya siku hiyo, basi ingelifikishwa kwetu kwa usahihi wake.

 

Tunapoliendea somo hili kutoka katika kipengele cha uoni wa taariykh (Historia), tunakuta kwamba Swahaba (Radhwiya Allaahu ‘anhum) hawakupatapo kusherehekea maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wala maadhimisho ya sikukuu ya Mi’iraaj wala za mwaka mpya wa Hijriyah. Zaidi ni kwamba walikuwa hawazitafuti tarehe hizi. Wamekhitalifiana kuhusiana na tarehe ya siku yake ya kuzaliwa, wametoa tarehe tofauti katika hilo kwasababu walijua kwamba hakuna ibada maalumu katika tarehe hizo. Inajulikana sana kwamba kizazi cha Swahaba na kizazi cha kwanza, ambacho kilikuwa na tabia bora kwa taifa, hawakupatapo kusherehekea siku hizi, imezushwa baada ya miaka mingi.

 

Miongoni mwa matukio ya maajabu, ni mtawala wa Irbil kusherehekea siku ya kuzaliwa Nabiy, mwaka mmoja tarehe nane ya mwezi Rabiy’ul Awwal na mwaka mwengine kwa tarehe kumi na mbili ya mwezi huo kama ambavyo alivyotilia maanani mgongano wa simulizi za Wanachuoni katika siku ya kuzaliwa! [Ibn Khallikaan, Juzuu ya 1, ukurasa 437].

 

 

Kizuizi Cha Saba

Tarehe ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ndio tarehe hiyo hiyo aliyofariki (Jumatatu 12 ya mwezi wa Rabiy’ul Awwal) hivyo, furaha kwa maadhimisho haya sio sahihi zaidi ya majonzi. [Kama ilivyosimuliwa na Wanachuoni kadhaa, mfano Ibn Al-Haaj Al-Maaliky na Al-Faakihaaniy].

 

Ibn Al-Haaj Al-Maaliky amesema kwamba: “Kitu kinachoshangaza zaidi katika sherehe zao ni kwamba, wanafanya hafla za nyimbo na furaha kwa kuzaliwa kwake katika siku hiyo, wakati huo huo amehamia katika heshima kuu huko mbinguni (kifo chake), ambayo inasimama kama ni huzuni isiyo na mfano ambayo halijapatapo taifa kukumbana nayo, kwa hivyo, na kwa mujibu wa mtindo wanaoufuata, basi wanahitajika kulia na kuonesha huzuni, badala ya kuimba na kuonesha furaha kila wakati.” [Al-Mudkhal 2/16].

 

 

Kizuizi Cha Nane

Inatambulika kwamba sherehe za siku ya kuzaliwa Nabiy zinaongezeka katika ardhi za Waislamu (na) zenye kuwemo Manaswara kama vile mataifa ya Misri na Shaam, wakati hao Manaswaara wanasherehekea Krismasi kama ni siku ya kuzaliwa kwa Yesu (Nabiy ‘Iysaa (‘Alayhis-salaam) na halikadhalika maadhimisho ya watu wa familia yake. Waislamu wanaziiga, ambayo ndio sababu ya zaidi ya kuenea uzushi huu miongoni mwa Waislamu.

Huo ni uthibitisho mwengine wa ahadi ya Nabiy iliyomo ndani ya Hadiyth yake:

((لَتَتَّبِعُنَّ سُنَنَ مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ شِبْرًا بِشِبْرٍ ، وَذِرَاعًا بِذِرَاعٍ ، حَتَّى لَوْ دَخَلُوا حُجْرَ ضَبٍّ لاتَّبَعْتُمُوهُم))  قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، فَمِنَ الْيَهُودِ وَالنَّصَارَى؟ قَالَ : ((فَمَن؟))

“Mtafuata mwenendo wa wale waliokua kabla yenu, kiganja kwa kiganja na mkono kwa mkono, hata iwapo kama wataingia katika shimo la kenge mtawafuata.)) Wakasema: “Ee Rasuli wa Allaah: (Unakusudia) Mayahudi na Manaswara? Akasema: ((Ni nani zaidi yao?)). [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Kuwaiga wao imefikia hadi kwamba Mwanachuoni As-Sakhaawiy kusema: “Kama ilivyo kwa wale wenye kuabudia msalaba walivyoichukua siku ya kuzaliwa kwa Nabiy wao kama ni sikukuku adhimu kabisa, hivyo Waislamu wapo na uhalali zaidi (kama ingelikuwa ni sahihi) kuichukua siku ya kuzaliwa kwa Nabiy kuwa ni maadhimisho. Lakini uigaji wao umekanwa na Mulla ‘Aliy Al-Qarri kwa kusema: “Ukweli kwamba: Waislamu wanahimizwa kutokubaliana nao na kutowafuata…” [Al-Mawrid Ar-Raawiy fiyl Mawlid An-Nabawiy: 29].

 

 

Kizuizi Cha Tisa

Mapenzi ya Rasuli wa Allaah hayawezi kufungamana na kusherehekea siku ya kuzaliwa kwake, isipokuwa tu kwa kufuata Sunnah yake, na kuifanya kuwa ni bora kuliko kitu chengine chochote. Ni lazima tutambuwe kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba wake (Radhwiya Allaahu ‘anhum) walikuwa ndio bora katika kumuabudia Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na ndio wachaji Allaah bora kwa ummah huu, bila ya (wao) kusherehekea siku ya kuzaliwa, (na kwa vile) walikuwa kama hivyo, (basi)  Dini yetu inatulazimisha kuwafuata wao.

 

Ukweli kwamba ni lazima turidhike na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) sio tu kwa siku moja, lakini kila siku. Ni lazima turidhike kwa kufanya yale ambayo ameyaamrisha na kuachana na yale ambayo ameyakataza… Hivyo ndivyo ilivyo, kuwa kuitilia nguvu imani yetu, tunapata uzuri na mafanikio katika maisha ya dunia hii na ya baadaye.

 

 

Kizuizi Cha Kumi

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kwamba:

((لا تُطْرُونِي كَمَا أَطْرَتِ النَّصَارَى ابْنَ مَرْيَمَ ، إِنَّمَا أَنَا عَبْدٌ ، فَقُولُوا: عَبْدَ اللَّهِ وَرَسُولَهُ . .))

“Msinitukuze kama ambavyo wanavyomtukuza Manaswaara mwana wa Maryam, hakika mimi ni mja wa (Allaah) Hivyo semeni: Mja wa Allaah na Rasuli Wake)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

Sherehe nyingi katika hizo zinavuka mpaka wa kumtukuza Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kwa hivyo kwenda kinyume na maamrisho yake.

 

Halikadhalika, inashangaza pia, kwamba hata Wanachuoni wanaotetea kusherehekea siku za kuzaliwa wanakubali kwamba kuna utukuzaji uliovuka mpaka katika kumtukuza Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambao unaweza kufikia katika ukafiri!  Haswa pale ambapo watu wamechupa mpaka katika mipaka yote na kutunga vitabu ambavyo ndani yake kuna Hadiyth za uongo za kutungwa zinazonasibishwa kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kwa mfano, ‘Abdullaah Al-Ghamariy, mmoja katika ma-Sufi wakubwa wa leo amesema kwamba:

 

“Vitabu kuhusiana na siku ya kuzaliwa Nabiy vimejaa Hadiyth zilizotungwa ambavyo vimekuja kuwa kanuni yenye kuendelea katika bongo za jamii ya watu! Ninataraji kuandika kitabu kuhusiana na siku ya kuzaliwa Nabiy lakini hakitakuwa na vitu viwili: Hadiyth zilizotungwa na maneno ya kishairi yaliyo mabaya.

 

Ninachotaka kusema ni kwamba kuchupa mpaka katika ibada ni kawaida kuwa kumezuiliwa ndani ya Uislamu kama ilivyo kwa Aayah ambayo maana yake itakuwa ni:

يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لَا تَغْلُوا فِي دِينِكُمْ وَلَا تَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ إِلَّا الْحَقَّ ۚ

Enyi Ahlal-Kitaabi! Msipindukie mipaka katika dini yenu, wala msiseme juu ya Allaah isipokuwa ukweli. [An-Nisaa: 171]

 

Na tunahimizwa kufanya hayo hayo. Zaidi ya hivyo, mtu yeyote anayemtukuza Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa jambo ambalo halijathibitishwa ndani ya Dini yetu, hivyo anaangukia katika maana ya Hadiyth ya Nabiy:

مَنْ كَذَبَ عليَّ متعمِّدًا فليتبوأ مقعَدَه مِنَ النَّارِ

((… na yeyote anayekusudia kunitungia uongo, basi na atafute makazi yake ndani ya moto.)) [Hadiyth sahihi iliyomo ndani ya vitabu vya Hadiyth vya Al-Bukhaariy na Muslim].”

 

Juu ya hivyo, maadili ya Nabiy hayafungamani kutokana na mambo ambayo yanaweza kustahamiliwa. Maadili haya ni ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na hivyo maana hii inaweza kuwa hatari kuweza kutumika kubadili Shari’ah yote. (Katika akili za baadhi ya watu, kwa upande mwengine Shari’ah ya Uislamu inamilikiwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa)). Suala hili ni kubwa hata kwamba Abu Muhammad Al-Juwainy, ambaye alikuwa ni baba wa Imaam Al-Haramayn alisema kuwa mtu mwenye kusema uongo katika Hadiyth kuwa ni ‘kafiri’… na kuongeza “Hivyo uchupaji mipaka wote na vitu vyenye kwenda nje zaidi ya mipaka ni lazima vichomwe moto, ama si hivyo, wamiliki wake wataunguzwa ndani ya moto! “… Ee Rabb, tusamehe… (Katika kuiokosoa Qaswiydah ya Burdah ya Al-Buswayriy – Ushairi wa kumtukuza Nabiy).

 

Wanaendelea katika mambo yao ya kukamilisha hafla zao za kusherehekea siku ya kuzaliwa Nabiy pamoja na misamiati ya ukafiri na maombi yenye ukafiri. Na hakuna nguvu wala hila isipokuwa kwa Allaah…

 

 

Kizuizi Cha Kumi Na Moja

Kinachotokea katika Mawlid miongoni mwa mambo ya ufisadi yanayoonekana kwa uwazi na kila mtu, ufisadi unaotokea ni kama ifuatavyo:

 

Wanawashutumu watu wengine wasiokubaliana na sherehe ya siku za kuzaliwa (Mawlid) kwamba hawampendi Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), wakisahau kwamba kumuheshimu zaidi na kumpenda yamo ndani ya kufuata Sunnah na kukamatana na yale yaliyopokelewa na kufuatwa kutoka kwa wema waliotangulia, na kuachana na uzushi na yaliyochomekwa katika Dini.

 

Halikadhalika, kucheza na kutikisa vichwa na mabega na kuyumbayumba huku na kule kama wacheza dansi, pamoja na nyiradi za kutungwa na nyimbo zenye kuvuka mipaka na visa vya kutungwa…

 

Katika jambo hili, Shaykh ‘Aliy Mahfuudh wa Al-Azhar amesema: “Kuna ufisadi wa matumizi na uharibifu wa vitu na wakati…” [Al-Ibdaa’ 324]. Ninaongezea, kwamba uharibifu kama huo wa muda na pesa, kwa mujibu wa kanuni za Uislamu, unakatazwa na kutambulika kuwa ni dhambi mbaya hata kama litafanyika katika wakati ambao tendo hilo litaonekana linaruhusiwa alimuradi tu linapelekea katika matendo yenye kukatazwa.

 

 

Kizuizi Cha Kumi Na Mbili

Kuna makubaliano ya Waislamu kwamba (kusherehekea) siku ya kuzaliwa ya Nabiy ni uzushi uliongezwa katika Dini ya Uislamu, lakini Wanachuoni wametofautiana kuhusiana na asili yake iwapo ni nzuri au jambo baya. Wanachuoni wachache wameridhia kusema kwamba uzushi ulio mzuri (bid’atun hasanah) kwa utashi wao – kama walivyoona wao.

 

Lakini wengi wa Wanachuoni wenye msimamo madhubuti, wa kale na wa sasa, wamekubaliana kwamba kuadhimisha sherehe ya kuzaliwa ni jambo ambalo limekatazwa ndani ya Uislamu. Ni dhambi (Haramu), kwa mujibu wa ushahidi wa Shari’ah za Kiislamu ambazo zinakataza uzushi wowote katika matendo ya ibada.

 

Bila ya shaka sikukuu na sherehe zinaibuka kutokana na Dini ambayo haina sherehe za kuzaliwa hata kidogo. Hivyo Wanachuoni wengi wamekataza kufungua mlango wazi kwa uovu fulani. Ni jambo ambalo halijapatapo kutendwa na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) au Swahaba zake wala wema waliofuatia, au kizazi baada ya kizazi!

 

Kwa kutilia maanani kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakupatapo kutenganisha baina ya uzushi mzuri na uzushi mwengine bali alisema kwamba: “Kila uzushi ni upotovu.”

 

Imaam Maalik amesema kwamba: “Kila anayezusha uzushi ambao anadhani kuwa ni mzuri, atakuwa anadai kwamba Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekiuka ujumbe alioletewa kwa sababu Allaah Anasema:

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا ۚ

Leo Nimekukamilishieni Dini yenu, na Nimekutimizieni neema Yangu, na Nimekuridhieni Uislamu uwe Dini yenu. [Al-Maaidah: 3].

 

Hivyo, lile ambalo halikuwa sehemu ya Dini ya Uislamu katika siku ile (zama za Nabiy), kamwe haitakuwa sehemu ya Dini katika siku nyengine (zama zozote zingine).” [Al-I’tiswaam, Ash-Shaatwibiy].

 

 

Baadhi Ya Wanachuoni Waliohukumu Kwamba Sherehe Ya Kuzaliwa Mtume (Mawlid) Ni Uzushi:

 

Imaam Ash-Shaatwibiy ndani ya kitabu chake cha Al-I’tiswaam (1/34) ambapo alitaja ndani ya kurasa zake za mwanzo baadhi ya aina za uzushi, akihusisha sherehe ya kuzaliwa Mtume kuwa miongoni mwao, akakemea sana kitendo hicho. 

 

Imaam Al-Faakihaaniy kakemea sana kitendo cha Mawlid katika Risaalah yake maalum. 8/9.

 

Imaam Al-Haj Al-Maaliky kakemea naye Mawlid na kasema bid’ah katika kitabu Al-Mudkhal, 2, 11/12.

 

Mwanachuoni wa India, Abu Atw-Twayyib Shamsul-Haq Al-Adhwiym Abaadiy, naye kasema Mawlid ni bid’ah, na Shaykh wake; Bashiyrud-Diyn Qannuujiy, ambaye ameandika kitabu kwa lengo hilo, alichokiita “Ghaayatul Kalaam fiy Ibtwaal ‘amal Al-Mawlid wal-Qiyaam”. Angalia sharh yake ya Hadiyth sahihi: “Yeyote anayezua katika Dini yetu katika yale ambayo sio (asili) katika hiyo (Diyn), halitakubaliwa”, Iliyopo katika Sunan Ad-Daaraqutwniy.

 

Mwanachuoni Abu ‘Abdillaah Al-Haffaar Al-Maalikiy kutoka Morocco amesema kwamba: (Sherehe ya kuzaliwa Mtume haikuwahi kufanywa na kizazi cha wamchao Allaah baada ya Nabiy (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ambao ni Swahaba wake. Hawakupatapo kuitofautisha na nyakati nyengine za usiku kwa kazi nyengine yoyote. Kwamba wamejifunza kutoka kwa Nabiy (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ambaye hakupatapo kufanya ibada kwa Mola wake isipokuwa tu kwa yale Aliyomshushia.) [Al-Mi’yaar Al-Mu’arab. 7/99].

 

Mwanachuoni mwenye kuheshimika Ibn ‘Uthaymiyn amesema kwamba: “Wanafanya sherehe za kuzaliwa Mtume kwasababu – kama wanavyosema – wanampenda Nabiy (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Sisi tunasema: “Karibuni “kama mnampenda”, na karibuni “kama mnapenda kufanya sherehe za maadhimisho yake, lakini, kuweni na tahadhari kwamba kuna mizani iliyoruhusiwa na Rabb wa ulimwengu, Mbora wa Mahakimu ambaye amesema ndani ya Aayah Yake…

 قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ 

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi, Atakupendeni Allaah na Atakughufurieni dhambi zenu. Na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Al-‘Imraan: 31].

 

Kwa hivyo kama mtu ni mtiifu katika kudai kuonesha mapenzi ya Nabiy (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ni lazima amfuate (Sunnah yake), kinyume chake ni anasema uongo na wala hampendi Nabiy (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa sababu mizani hii ndio mizani ya imani na haki. Sasa tuangalie hii sherehe ya kuzaliwa, je, imefanywa na Nabiy (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)? Je, imefanywa na Makhalifa waongofu? Je, imefanywa na Swahaba wengine? Je, imefanywa na kizazi chema kilichofuata?

 

Jibu kwa masuala yote haya ni hakika kuwa “Hapana” na yeyote anayedai kuwa na jibu jengine, sisi tutasema: Tupe ushahidi wako kama wewe ni muadilifu).  – Tovuti ya Shaykh Ibn ‘Uthaymiyn.

 

 

Mwisho

 

Ninamuomba Rabb wangu Allaah, kuzikubali kurasa hizi chache kama ni kazi iliyotolewa katika njia yake. Ninaomba kwamba wanufaike nayo wengine na hilo ni tarajio langu kubwa. Zaidi ninamuomba Allaah hifadhi. Yeye ndiye Mtukufu, Yaa Allaah, Rabb wangu, tuimarishe katika Haki. Zifanye kazi zetu ziwe kwa ajili tu ya kutafuta radhi zako. Yaa Allaah, wewe ni Mkwasi na Mwenye kuongoa katika njia sahihi. Maombi yangu ya mwisho ni kwamba utukufu na shukrani zote ni za Allaah, Rabb wa viumbe vyote.

 

 

Na Miongoni Mwa Wanachuoni Waliopinga Mawlid (Ambao Hawakutajwa Na Mwandishi Hapo Juu)

 

Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah - Iqtidhwaa As-Swiraatw Al-Mustaqiym (2/619) na Majmu’ al-Fataawa (1/312)

 

Shaykh Taajud-Diyn ‘Umar bin ‘Aliy Al-Lakhmiy Al-Iskandariyy (Mwanachuoni wa Madh-hab ya Al-Malikiy Alexandria mwaka 734H) - Al-Mawruwd fiy Kalaami ‘alaa ‘amal al-Mawlid

 

Shaykh Muhammad Bukhiyt al-Mutwiy’iy al-Hanafiyy (Mufti wa Diyaar Al-Miswriyyah)

 

Shaykh ‘Aliy Mahfuwdhw – katika kitabu: Al-Ibdaa’ fiy Midhwaari al-Ibtidaa’

 

Shaykh Muhammad bin ‘Abdis-Salaam Khudhwar Ash-Shaqiyri – Katika kitabu chake: As-Sunan wal-Mubtadi’aati

 

Shaykhul-Islaam Al-Mujaddid Muhammad bin ‘Abdil-Wahhaab

 

Al-‘Allaamah Shaykh ‘Abdur-Rahmaan Aal Shaykh – Katika: Ad-Durar As-Sanniyyah.

 

Al-‘Allaamah Shaykh Muhammad bin Ibraahiym – Risala yake kukanusha kitendo cha Mawlid. Taz. Majmu’ Fataawa yake (3/48-95). Imekusanya Fataawa mbali mbali kuhusu Mawlid.

 

Al-‘Allaamah Shaykh ‘Abdullaah bin Muhammad bin Humayd – Risaalah yake: Hidaayah An-Naasik Ilaa Ahammil-Manaasik.

 

‘Allaamah Shaykh ‘Abdul-‘Aziyz bin Baaz – Risaalah yake: Hukmu Al-Ihtifaal Bil-Mawlidin-Nabawiyy.

 

‘Allaamah Shaykh Muhammad Naaswirud-Diyn Al-Albaaniy

 

‘Allaamah Shaykh Muhammad bin Swaalih Al-‘Uthaymiyn

 

‘Allaamah Shaykh Swaalih bin Fawzaan Al-Fawzaan

 

Shaykh Humuwd bin ‘Abdullaah At-Tuwayjiriy katika Risaalah yake: Ar-Radd Al-Qawiyyi ‘alaa Ar-Rifaa’iy wal-Majhuwl wabn ‘Alawiyy wa Bayaan Akhtwaaihim fil-Mawlid An-Nabawiyy

 

Shaykh Ismaaiyl Al-Answaariyy – Risaalah yake: Al-Qawl Al-Faswli fiy Hukm Al-Ihtifaal bi-Mawlidi Khayrir-Rusul

 

‘Allaamah Shaykh Bakr Abuu Zayd

 

 

 

Share