Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Makosa Kuwaita Mashemeji Na Wakwe Kuwa Ni Ndugu Wa Nasaba

 
Ni Makosa Kuwaita Mashemeji Na Wakwe Kuwa Ni Ndugu Wa Nasaba
 
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
 
 
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
 
 
"Watu wengi wa kawaida (wasio na elimu) hawafahamu maana ya neno 'wenye nasaba' au 'ndugu' isipokuwa wanadhani jamaa wa mume na mke!
Hadi inafikia mtu anasema, 'hao ni jamaa zangu wa nasaba au ni ndugu zangu' kwa sababu tu yeye kaoa kwao! Hili ni kosa kilugha na kishariy'ah.
Kwani kwa hakika, jamaa wa nasaba ni wale walio karibu upande wa baba au upande wa mama.
Na kadhaalika 'ndugu' vilevile ni wale wenye ukaribu na upande wa baba au upande wa mama.
 
Ama jamaa wa upande wa mume na mke, hao huitwa 'mashemeji na wakwe' na si ndugu wa nasaba.
 
Amesema Aliyetuka:
 
"Naye Ndiye Aliyeumba mtu kutokana na maji, kisha Akamjaalia kuwa na unasaba wa damu na uhusiano wa ndoa. Na Rabb (Mola) wako daima ni Qadiyra (Mweza wa yote."
 
Kajaalia uhusiano baina ya wanaadamu kwa hizi amri mbili: 'Nasaba (uhusiano wa damu)', na 'Ushemeji na Ukwe (uhusiano wa ndoa)'.
 
 
[Nuwru 'Alaa Ad-Darb, 6/11]
 
 
 
Share