Ndizi Mbichi Za Supu Ya Nyama Ng’ombe

 

Vipimo

Ndizi mbichi - Kisia

Nyama ng’ombe  -  ½ kilo

Pilipili ya kusaga  -  1 kijiko cha chai

Tangawizi ya kusaga - 2 vijiko vya supu

Thomu (garlic/saumu) - 1 kijiko cha supu

Bizari mchuzi -  1 kijiko cha chai

Nazi ya unga (ukipenda kuongezea) - 2 vijiko cha supu               

Chumvi - Kiasi

Ndimu  - 1 kamua                                                          

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Weka nyama ng’ombe katika sufuria, tia tangawizi, thomu, pilipili mbichi, bizari, chumvi. Roweka kidogo ukipenda kisha ikaushe yenyewe kwa maji yake
  2. Ongezea maji ya kiasi yasizidi mno, kisha funika na chemsha.
  3. Menya ndizi, ukatekate.
  4. Nyama ikikaribia kuiva, weka ndizi uendelee kupika mpaka viive vyote.
  5. Tia nazi ya unga kidogo tu ukipenda. Koleza kwa bizari mchuzi, pilipili, na ndimu
  6. Epua mimina katika chombo cha kupakulia zikiwa tayari.

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

Share