Mwanamke Kupaka Piko Katika Nywele

 

Mwanamke Kupaka Piko Katika Nywele

 

Alhidaaya.com 

 

 

SWALI:

 

Naitwa …….  kutokea ....... ningefurahi kuelimishwa juu ya uhalali wa kupaka Piko kwa mwanaume na mwanamke. Inshaa Allah majibu yange kuwa katika vipengele vifutavyo;

a) Je, nihalali kwa mwanaume kupaka piko katiki nywele zao?
b) Je, kutoka kipengele a kama jibu litakuwa Haifai ni kitu gani mwanaume anaweza paka katika nywele zake kama urembo kutoa Hina?
c)   Inajuzi kwa mwanamke kujipamba kwa pambo la Piko.
Inshaallah ni matumaini yangu kwa uwezo wa Allaah (s.w) mtanijibu

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Kwanza, tunakukumbusha kutokufupisha kumtukuza Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  nk. Faidika na maelezo yake katika kiungo kifuatacho:

 

Hukmu Ya Kufupisha Thanaa (Kumtukuza Allaah) Na Kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) Na Maamkizi Ya Kiislam

 

Ama kuhusu swali lako la kwanza, haifai kwa mwanamme kupaka piko kwenye nywele kwani piko ina sifa ya rangi nyeusi na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kakataza kupaka rangi nyeusi kwenye nywele (na ndevu pia zinaingia).

 

 

Na piko si kama hinna ambayo inafaa na inaruhusiwa kwa mwanamme kupaka nyweleni au ndevuni.

 

 

Piko vilevile ina kemikali ambayo ina madhara. Na chenye madhara chochote hakifai matumizi yake kama Hadiyth ya Rasuli inayoeleza makatazo ya kujidhuru:

"Hakuna kujidhuru wala kudhuriana" (Ibn Maajah na Ad-Daraqutwniy, nayo ni Hasan).

 

 

Ama swali lako la pili na la tatu kuna majibu ndani ya kiungo kifuatacho:

 

Bi Harusi Kujipamba Katika Mipaka Ya Sheria

 

Na Allaah Anajua zaidi

Share