Moussaka Bilingani Kwa Sosi Ya Nyanya Beshamel Na Jibini

Moussaka Bilingani Kwa Sosi Ya Nyanya  Beshamel Na Jibini

Vipimo

Nyama ya kusaga - ¼ kilo

Bilingani - 4 kubwa

Kitunguu kilokatwakatwa - 2

Nyanya – katakakata  - 4

Pilipili boga (capsicum) - 1

Tangawizi mbichi ilokunwa au kusagwa - 1 kipande

Nyanya kopo - 1 kijiko cha supu

Herbs ya oregano - 1 kijiko cha chai

Nanaa kavu (dry mint) - ½ kijiko cha chai

Pilipili manga - 1 kijiko cha chai

Chumvi  - kiasi

Jibini ya cheddar au mazorella - 500 gms

Mafuta - 3 vijiko vya kulia

Mafuta ya kukaangia bilingani - Kiasi

Sosi ya beshamel:

Unga -  vijiko 3 vya kulia

Siagi -  vijiko 2 vya kulia

Maziwa  - kiasi gilasi 3

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Osha nyama kiasi uichuje
  2. Kata bilingani slices ndefu. Kaanga katika mafuta mengi yaliyo yamoto, Epua uchuje mafuta.
  3. Weka mafuta vijiko 3 katika sufuria, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi kidogo.
  4. Tia nyama, na tangawizi uchanganye vizuri, kakaanga kidogo.
  5. Tia nyanya na viungo vyote isipokuwa jibini. Kaanga kidogo. Epua
  6. Panga nusu ya slesi za bilingani katika bakuli la kupikia ndani ya oven.

    7. Mwagia sosi juu yake kisha kuna jibini (cheese) umwagie juu yake.

    8. Panga tena slesi za bilingani kisha mwagia sosi ya beshamel kisha jibini tena.

    9. Weka ndani ya oven upike (bake) kwa moto mdogo wa kiasi mpaka igeuke rangi kidogo.

    10. Epua ipoe, ikiwa tayari.

Namna ya kutengeneza sosi ya beshamel

  1. Weka siagi katika sufuria, tia unga weka katika moto, kaanga ugeuke rangi.Tia maziwa
  2. na kidonge cha supu ukoroge usiachie mkono mpaka uive.
  3. Epua utumie kumwagia katika moussaka au pasta yoyote ile.

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

Share