Sandwichi Ya Samaki Tuna Mayonaise Na Jibini Ya Mazorella

Sandwichi Ya Samaki Tuna Mayonaise Na Jibini Ya Mazorella 

 

Vipimo

Slaisi za mkate - 12 kiasi

Samaki wa tuna - 2 vibati

Jibini Mazorella (Cheese) - Kiasi

Mayonaise - kiasi

Kitunguu katakata - 1

Nyanya/tungule katakata - 1

Pilipili manga ya unga - 1 kijiko cha chai

Herbs za oregano - 1 kijiko cha chai

Herbs za nanaa (mint) - 1 kijiko cha chai

Mafuta - 3 vijiko cha kulia

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Weka mafuta katika sufuria, kaanga kitunguu kiasi kilainike, weka nyanya ukaange.
  2. Tia samaki wa tuna aliyechambuliwa.
  3. Weka viungo na herbs zote changanya vizuri, epua.
  4. Panga slaisi za mikate katika treya ya kuingia katika oven.
  5. Pakaza mayonaise, kisha tia sosi ya tuna katika slaisi zote.
  6. Mwagia jibini ya mazorella kisha weka katika oven uchome (grill) moto mdogo mdogo.
  7. Epua ikiwa tayari

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

 

 

 

 

 

Share