Slesi Za Jibini Ya Mozzarella Na Thomu

Slesi Za Jibini Ya Mozzarella Na Thomu  

   

Vipimo 

Slesi Za Mikate -  12 

Jibini Ya Mozzarella iliyokunwa - 1 kikombe 

Kitunguu saumu(Thomu/galic) ya unga - 2 vijiko vya supu 

Siagi  - kiasi 

Oregano - ½ kijiko cha chai 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Paka siagi  slesi za mkate.
  2. Nyunyizia Jibini ya mozzarella iliyokunwa (grated cheese)
  3. Nyunyizia thomu na oregano.
  4. Weka katika treya na choma katika oven kwa moto wa juu (grill)
  5. Zinapogeuka rangi na jibini kuyayuka toa katika oveni, panga kwenye sahani.

 

 

Share