Imaam Ahmad: Alivyopambana Na Ibliys Katika Sakaraatul-Mawt!

 

Imaam Ahmad Bin Hanbal Alivyopambana Na Ibliys Katika Sakaraatul-Mawt!

 

‘Abdullaah Bin Ahmad Bin Hanbal (Rahimahuma-Allaah)

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

‘Abdullaah Ahmad bin Hanbal (Rahimahuma-Allaah) amesema:

 

“Mauti yalipomkaribia baba yangu wakati nimekaa karibu yake, alikuwa akizima na kuamka huku akisema: “Bado! Bado!”

 

Alifanya hivyo mara kwanza kisha tena mara ya pili na mara ya tatu nikamuuliza:  “Ee baba yangu! Unakusudia nini hayo usemayo wakati huu?” Akajibu: “Mwanangu mpenzi! Hutambui, lakini Ibliys aliyelaaniwa alinisimamia miguuni mwangu akijiuma vidole vyake huku akisema: “Ee Ahmad! Umenikwepa (mkamato wangu wa kukupotosha), ndio nikawa namjibu bado! Bado! Mpaka nife.”

 

 

[Hilyatul-Awliyaa (/91830]

 

 

Share