Sitta Shawwaal: Ikiwa Deni La Ramadhwaan Zaidi Ya Mwezi Afunge Deni Kwanza Au Sita Shawwaal?

 

Ikiwa Deni La (Swiyaam Za) Ramadhwaan Ni Zaidi Ya Mwezi

Afunge Deni Kwanza  u Sita Shawwaal?

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Je ikiwa mwanamke alijifungua (kazaa) yaani kapata mtoto kabla ya ramadhani na ramadhani ikamkutia bado hajakooga arubaini (siku 40 baada ya kujifungua) na ikawa siku ya edi-el fitri ndio siku yake ya mwisho, na akamua kuwa siku inayofuata aanza kulipa (yaani mwezi pili mfunguo mosi)ramadhani na wakati huo huo anataka afunge sitatul shawwali, na iwapo kama atafunga ramadhani siku 29 au 30, ataikosa sitatul shawwal je anaweza kuanza sitatul shawwal, badae ndio akanza kufunga ramadhani? na je ni lazima akianza kufunga ramadhani  azifuatanishe zote siku 29/30 au anaweza kufunga taratibu taratibu?

Natunguliza shukurani kwa majibu, na nitafurahi kama nitapata majibu kabla ya ramadhani kwisha, kwani hiyo kesi nakabiliana nayo nikiwa nje ya nchi (Uchina)

AS-SALAAM ALAYKUM

 

 

JIBU:

 

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Ikiwa ni hali kama hiyo uliyoitaja basi atakuwa ana 'udhuru wa kumchelewesha kufunga Sita Shawwaal, kwa hiyo hukumu yake ni vile vile kwamba kwanza amalize deni la Ramadhwaan mpaka alimalize, na atakapomaliza deni na ukaingia mwezi wa pili yaani Dhul-Qa’dah basi afunge Swawm za Sita Shawwaal katika mwezi huo na atapata fadhila zake.    Lakini atakayeuacha mwezi wa Shawwaal kupita bila ya kufunga na bila ya 'udhuru wowote, basi hatopata thawabu za Sita Shawwaal ikiwa atazifunga katika mwezi wa Dhul-Qa’dah.

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn alipoulizwa kuhusu mas-ala haya , alimalizia kujibu   kwa kusema: "Ikiwa mfano mwanamke aliyetoka katika uzazi amelipa deni lake lote katika mwezi wa Shawwaal, kisha ukaingia mwezi wa Dhul-Qa’dah nayeye anataka kufunga Sita Shawwaal apate fadhila zake, basi afunge Sita Shawwaal katika mwezi huo wa Dhul-Qa’dah ili apate thawabu zake, kwa sababu amezichelewesha (funga za Sita Shawwaal) kutokana na 'uhduru (sababu) muhimu.  

[Majmu'u ya Fataawa 20/19] 

 

 

Kuhusu utaratibu wa kufunga, kama tulivyosema hapo juu kwamba ikiwa mtu ana niyyah ya kufunga na Sita Shawwaal na yeye ana deni la mwezi mzima, basi  afunge deni lake katika mwezi wa Shawwaal bila ya kuziwacha siku kupita ili aunganishe na Sita Shawwaal hata kama umeingia mwezi wa pili.  Lakini kama mtu hana niyyah ya kufunga Sita Shawwaal, basi sio lazima kulipa deni lake kwa mfululizo, bali anaweza kufunga na kupumzika na anaweza pia kumalizia deni lake katika miezi mingine.

 

Bonyeza viungo vifuatavyo upate faida ziyada:

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share