Kusoma Tawassul Inafaa Katika Hedhi?

 

Kusoma Tawassul Inafaa Katika Hedhi?

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Is one allowed to recite (read) "Tawasul" when they are on their periods? Some people read it every thursday night and usually even at "taaziya's".  Mtu akifa, jamaa husoma tawassul alafu wakamtiliya maiti fatha.  Also, for example, I have it on tape and I would usually play it in the car and my children and I will follow along.

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Bila ya shaka hiyo tawassul ni ile inayojulikana kama Wasiylatush-Shaafiy au Wasiylatun-Nabaahaniy  ambayo ‘Ulamaa wamefutu kuwa haifai na ni bid’ah.

 

Bonyeza kiungo kifutacho upate maelezo bayana:

 

 29-Tawassul Za Shirki Kufru Na Bid’ah: Kutawassal Kwa Wasiylatush-Shaafiy

 

Haifai kabisa na unapaswa kuachana nayo na badala yake ushikilie kusoma Qur-aan na nyiradi au du’aa zilizothibiti katika Qur-aan na Sunnah,, na badala ya kuwasikilizisha watoto wako hiyo du'aa ya bid'ah, wasikilizishe watoto wako Qur-aan, kwa sababu Qur-aan ni khayr na ni bora na ni muhimu na yenye faida zaidi na manufaa kwako na kwa Aakhirah yako.

Fanya na fuata mambo yaliyothibiti kishariy'ah na usifuate mazoea au kuona watu wanafanya au kutenda kama ada na mazoea.

 

Jizoeshe na wanao kusoma Qur-aan sana na kuisikiliza sana na kusoma du'aa na adhkaar zilizothibiti za asubuhi na jioni na za minaasabah mbalimbali.

Hayo yana faida kwako na khayr na ndiyo yenye kuchumwa thawabu, na hayo ya bid’ah ni kinyume chake kutokupata thawabu zozote zile na juu ya hivyo kuchuma dhambi.

 

Inakupasa kuwalea watoto katika mafunzo sahihi ili waokoke na bid’ah ili wabakie katika mwenendo wa Salafus-Swaalih (Wema waliotangulia) na ili waokoke na makundi potofu.

 

Suala la kusomwa Al-Faatihah katika shughuli mbali mbali kama za misiba n.k pia halikuthibiti katika Shariy’ah, hivyo nalo ni bid’ah.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share